# Kujipanga vema kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa halmashauri ya Arusha kisekta.
# Wameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya emaendeleo inakwenda vizuri katika kata zote 27 ikiwemo miradi ya Elimu kata za Oldonyowas, Mlangarini, Bangata, Miradi ya Maji Bwawani, Lovilukuny, Likamba na mradi wa maji wa Vijiji vitano,Miradi ya Afya Mbuyuni na Manyire pamoja na miradi ya TASAF.
# Wamewapongeza wataalamu kwa kuwezesha ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba kwa kushika nafasi ya 21 kitaifa na nafasi ya 2 kimkoa.
# Wamewaomba wadau kujitokeza kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wanaotarajiwa kuchaguliwa kujiunga na kadato cha kwanza, mapema mwezi Januari 2019, kutokana ongezeko la ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba imesababisha uhitaji wa vyumba vya madarasa 109.
# Kwenye kata na vijiji ambavyo havina Maafisa Watendaji kutokana na sababu mbalimbalo, wameomba kuwatumia wataalamu wa fani nyingine kwenye maeneo husika na kukaimishwa nafasi hizo ili kuepuka kazi za maeneo hayo kutokusimama.
# Maeneo yenye migogoro ya mipaka yatafutiwe ufumbuzi kwa haraka kuepuka migogoro hiyo kuwa mikubwa.
# Wataalamu kuwaelimisha wananchi wanaofanya biashara ya mboga mboga na matunda karibu na mto katika soko la Ngaramtoni, kuchukua tahadhari kutokana na kufanya biadhara katika eneo hatarishi na kutambua madhara yanayoweza kuwapata endapo patatokea ajali ya gari katika eneo hilo na kuwataka wananchi hao kuhama katika eneo hilo na kuhamia eneo la soko halali.
Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Wilson Mahera, akizungumza na wajumbe wa mkutano wa Baraza la Madiwani juu ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ndani ya halmashauri hiyo.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakifuatilia mijadala inayoendelea wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la kuwasilisha taarifa za kata, kwa kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2018/19

Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.