• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ZOEZI ZA UIBUAJI KAYA ZA KUINGIZWA KWENYE AWAMU YA PILI MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI -TASAF AWAMU YA TATU LAANZA RASMI ARUSHA DC

Posted on: August 17th, 2021

Na. Elinipa Lupembe.

Zoezi la kitaifa la kubaini kaya zenye vigezo vya kuingia kwenye mpango wa Kunusuru kaya masikini, katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi unaotekelezwa na TASAF awamu ya tatu kwa mwaka 2020-2025, limeanza rasmi katika vijiji 43 vya halmasahuri ya Arusha, vijiji ambavyo havikuwa kwenye mpango katika awamu ya kwanza ya mradi huo.

Jumla ya wawezeshaji 43 (PAA FACILITATOR) wametawanyika katika vijiji hivyo 43, wakielekeza viongozi ngazi ya vijiji na vitongoji pamoja na wananchi vigezo vya kuziibua kaya hizo, kwa kuzingatia vigezo vya kitaifa na vigezo vya  na vigezo vya eneo husika, zoezi linalofanyika kupitia mikutano ya serikali za vijiji na mikutano maalumu ya vijiji, huku vigezo vya upimaji vikiwekwa wazi kwa kila mwananchi

Katika maeneo mengi ya vijiji husika, wananchi wamejitokeza kwa wingi, kushiriki zoezi hili muhimu kwao, lenye lengo la kuziibua kaya hizo na kuziwesha kaya zisizo na uwezo wa kujikimu kimaisha, kuingizwa kwenye mpango wa serikali wa kupambana na umasikini kwa kuziwezesha kaya hizokujiinua kimaisha pamoja na kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini uliokithiri kwenye jamii.

Hata hivyo baada ya kaya hizo kupitishwa na wananchi kwenye mkutano mkuu wa kijiji, wawezeshaji watalazimika kupita kwenye makazi ya kaya zilizoibuliwa (kaya kwa kaya), ili kuorodhesha majina ya wanakaya hao pamoja na kudodosa hali halisi za kijamii na kiuchumi za kaya hizo, lengo likiwa ni kujiridhisha na uwepo wa kaya hizo katika eneo husika.

Zoezi hilo la wazi na linategemea kufanyika kwa takribani siku kumi kwenye vijiji hivyo vya halmashauri ya Arusha, hivyo wananchi ambao majina yao yatapitishwa kwenye mkutano mkuu wa kijiji na Vitongoji, watalazimika kutoa ushirikiano mkubwa kwa wawezeshaji hao, ili kupata kaya zenye vigezo halisi vilivyoainishwa na si vinginevyo, ili kuepuka malalamiko sambamba na kutimiza adhma ya serikali ya kupambana na umasikini katika jamii ya watanzania. 

Aidha kaya zitakazoibuliwa zinatakiwa, kuwepo nyumbani  kwa zile siku zilizokubalika na viongozi wa vijiji kwa kushirikiana na  wawezeshaji wa TASAF, ili kaya hizo ziweze kutoa taarifa sahihi za kaya zao, ikiwemo idadi ya wanakaya, majina sahihi ya wanakaya, majina sahihi ya shule wanazosoma watoto wao, majina shahihi ya vituo vya afya wanavyotumia kupelekwa watoto wanaohudhuria kliniki, watoto wenye umri wa mwaka sifuri mpaka miaka mitano.

ARUSHA DC KAZI INAENDELEA✍✍


Mwenyekiti wa kijiji cha Ilkerini mheshimiwa Sanaek Soye, akifungua mkutano maalumu wa  kijiji, tayari kwa uibuaji wa kaya za kuingiwa kwenye mradi wa Mapngo wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na TASAF awamu ya tatu 2020 -2025.

Wananchi wa kitongoji cha Parselian kijiji cha Ilkerin, wakiwa tayari kuanza kutaja majina ya kaya zenye sifa za kuingizwa kwenye awamu ya pili ya mradi wa kaya maskini TASAF awamu ya tatu, zoezi lililofanyika wakati wa mkutano maalum wa kijiji cha Ilekerin kata ya Kisongo.


Mjumbee wa serikali ya kijiji cha Ilkerini kata ya Kisongo (jina halikuweza kuapatikana) akiwaelezea wananchi wa Ilkerin umuhimu wa kuibua kaya zenye sifa, wakati wa mkutano maalumu wa kijiji wa kuibua kaya zenye uhitaji kuingizwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini.

Wananchi katika mkutano wa kijiji cha Engutukoiti kata ya Losinoni.


Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Engutukoiti wakiwa kwenye mkutano wa kijiji.

Wajumbe wa serikali ya kijiji cha Engutukoit kata ya Losinoni wakilamkiapo cha utii wa kusimamia kazi ya uibuaji kaya zenye uhitaji katika kijiji chao.


Mwezeshaji akiendelea kutoa maelekzo kwa wananchi juu ya uibuji kaya za kuingiankwenye mradi wa kunusuru kaya masikini na TASAF awamu ya tatu, kwenye Mkutano wa wananchi wa kijiji cha Likamba kata ya Musa

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.