Mradi wa Ujenzi na upanuzi wa Miundombinu ya Kituo cha Afya cha Nduruma ni moja kati ya vituo vya Afya 44 nchini vinavyojengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Canada kwa lengo la kuboresha Vituo vya Afya nchini.
Halmashuri ya Arusha imepokea kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa Kituo cha Afya cha Nduruma na utekelezaji wake unafanyika kwa kipindi cha robo ya pili ya kuanzia mwezi Oktoba – Disemba kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Lengo la Serikali ni kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha Afya chenye hadhi ya Nyota tano kwa kuboresha vituo hivyo vya Afya ili viweze kutoa huduma za haraka na kwa wakati lengo likiwa ni kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.
Kiasi hicho cha fedha kinatumika kujenga jengo la Maabara kwa ajili ya vipimo, jengo la Mama na Mtoto 'Maternity Ward', jengo la kuhifadhia Maiti 'Mortuary', jengo la kuchomea taka 'Incinerator', nyumba ya Mganga pamoja na umaliziaji wa jengo la upasuaji 'Operation Theater'.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.