• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DED Arusha DC ateta na Watumishi

Posted on: September 10th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, amewataka watumishi wa halmashauri hiyo, kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano kama timu, bila kujali nafasi walizonazo, ili kufikia malengo ya yaliyoaanishwa kwenye mpango mkakati wa halmashauri hiyo.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji alipokutana na watumishi wa sekta zote za halmshauri hiyo, katika kikao kazi cha kawaida, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, mwanzoni mwa wiki hii.

Mkurugenzi Dkt. Mahera, amefafanua kuwa lengo la kikao hicho ni kukumbushana wajibu na majumumu ya kila mtumishi, kwa kujengeana uelewa wa pamoja kwa watumishi wote katika uwajibikaji wenye tija ya kufikia malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi wa halmashauri hiyo pamoja na kujadili changamoto zinazokwamisha utendaji kazi.

Amewakumbusha watumishi hao, kutambua kuwa utumishi wa Umma ni dhamana waliyopewa na Serikali, na kuwataka kufanya kazi, kwa kuzingatia kanuni, sheria, taratibu na za utumishi wa umma pamoja na miongozo ya serikali, kwa kutumia taaluma zao katika kutekeleza majukumu yao, kwa kuzingatia haki na usawa.

"Serikali imewaamini na kuwapa dhamana ya kuwatumikia wananchi, tumieni taaluma zenu kutekeleza majukumu yenu, tushirikiane kama timu ili kuijenga Arusha DC na Serikali yetu kwa ujumla" amesema Dkt. Mahera.

Sambamba na hayo Dkt. Mahera amewaagiza Maafisa watendaji wa kata, kusimamia suala la usafi wa mazingira na kuhakikisha wananchi,  wanatozwa tozo stahiki za taka na kupewa risiti za fedha zilizolipiwa, sambamba na kuwachukulia hatua za kisheria, wananchi ambao wanakaidi na kunyanyasa wengine.

Naye Mkuu wa Idara ya Utumishi, halmashauri ya Arusha Hamis Mpume, amewaahidi watumishi hao kuendelea kusimamia haki zao, wajibu na usawa, na kuwakumbusha watumishi hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma ikiwa ni apamoja na kutekeleza wajibu wao na kuahidi kuwachukulia hatua watakaokwenda kinyume.

“Nina imani kila mtumishi anafahamu vizuri majukumu yake, niwatake kila mmoja wenu kuyatekeleza kazi zenu kwa ufanisi, naahidi kutenda haki kwa kila mtumishi, sitamuonea mtu lakini sitasita kumchukulia hatua stahiki mtumishi asiotekeleza majukumu yake"  amesema Mpume

Naye Afisa Mtendaji kata ya Mateves, Muyai Kivuyo,licha ya kumshukuru Mkurugenzi huyo,  kwa kukaa pamoja na kujadili changamoto zinazowakabili, wamemuomba mkurugenzi huyo kuwapa taarifa za shughuli za miradi ambozo huendelea katima kata zao ili wafahamu na kushiriki katika kufuatilia miradi hiyo.

Kikao kazi hicho kimewakutanisha, watumishi wa ngazi za kata, ikiwemo Maafisa watendaji kata, maafisa Ugani na Mifugo, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Afya, Maafisa Elimu kata, pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo.

Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo, kwenye kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa halmashauri hiyo.

Watumishi wa halmashauri ya Arusha, wakiwa kwenye kikao kazi, kwenye ukumbi  wa mikutano wa halmashauri hiyo.


Afisa Utumishi, halmashauri ya Arusha, Hamis Mpume, akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo, kwenye kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa halmashauri hiyo.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.