Na.Elinipa Lupembe
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii -TASAF kupitia mradi wa mpango wa kunusu kaya masikini, umewawezesha wanufaika wa mpango huo katika halmashauri ya Arusha, kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa kutumia ruzuku ya fedha wanazopata kila baada ya miezi miwili.
Wanufaiko hao wamekutwa na mwandishi wetu wakiendela kufanya biashara nje ya ofisi ya kijiji cha Ilkiding'a, wakati wanasubiri kupokea fedha zao za ruzuku ya TASAF, huku zoezi la uhawilishaji wa fedha za kaya masikini, likiendelea katika ofisi hizo, ikiwa ni ruzuku ya mwezi Mei na Juni 2021.
Waafanyabiashara hao ndogo ndogo wamekiri kuinua biashara zao kupitia fedha ndogo wanayoipokea kama ruzuku ya mpango wa kunusuru kaya masikini, mradi unatekelezwa na serikali kupitia mfuko wa maendeleo ya Jamii -TASAF, na kukiri kuwekeza fedha hizo kwenye biashara ndogo ndogo kama kuuza mitumba, vyomba na kuuza mbogamboga sokoni.
Loveness Rashid, mkazi wa kijiji cha Ilkiding'a na mnufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini amethibitisha kupata mtaji wake wa kuuza vyombo, kupitia fedha hizo za ruzuku na kuonheza kuwa japo pesa hizo ni kidogo lakini zinawawezesha kuendesha maisha na kuondokana na umasikini uliokithiti waliokuwa nao hapo awali.
"Ninauza vyombo kama unavyoviona hapa, na wateja wangu ni hawa hawa wanufaika wa mpango wa kaya masikini, tunaishukuru serikali yetu, tunamshukuru mama Samia, kwa kutuwezesha kupata pesa hizi, zimesaidia watu weng hapa kijijinii amabao hawana uwezo na hali duni za maisha, sasa hivi walau wanamaisha mazuri sio kama zamani" amesiaitiza Loveness
Naye Elinita Mollel, mfanyabiashara wa kuuza nguo za mitumba kwa kutembeza mitaani, amesema kuwa mtaji wa biashara hiyo umetokana na fedha za ruzuku ya TASAF, biashara amabyo anaitegemea kuendesha maisha ya familia yake na familia kwa ujumla.
Aidha mnufaika mwingine wa kijiji cha hicho hicho cha Ilkiding'a, na mfanyabiashara ya mboga wa soko la Samunge lajijini Afusha, Felista Moses Laizer, amesema kuwa licha ya kuwa anapokea kiasi kidogo cha fedha, kilimuwezesha kuanza biashara ya kuuza mboga sokoni, biashara ambayo imesaidia kumudu kuendesha maisha ya familia yake, huku pato la familia likipanda tofauti na hapo awali ambapo hali ya kiuchumi ilikuwa mbaya sana.
"Nilipokea hela ya TASAF kiasi nikatumia na shilingi elfu 10, nikatumia kama mtaji wa biashara yangu ya kuuza mboga, nanunua mboga kwa wakulima shambani na kuuza sokoni, TASAF imenisaidia , sikuwa na uwezo hata wa kupata huo mtaji wa elfu 10,kwa sasa hali ya maisha sio mbaya kama hapo zamani" amefafanua Felista.Hata hivyo Mratibu wa TASAF halmashauri ya Arusha, Grace Makema, amesema kuwa mpango huo wa kunusuru kaya masikini, umenufaisha familia nyingi ambazo hutumia fedha hizo kufanya biashara ndogo ndogo, tofauti na wale amabao hupoke pesa hizo na kula tu na kuwataka wanufaika hao kuendele kutumia kiasi cha fedha hizo kuwekeza kwenye biashara ndogo ndogo jambo ambalo litarahisisha hali za maisha yao.Mratibu huyyo ameeleza kuwa kwa kipinid cha mwezi Mei na Juni 2021, halmashauri imetoa ruzuku ya takribani shilingi milioni 284.4, kwenye jumla ya kaya 8167 katika vijiji 45 vilivyo kwenye mpango wa kunusu kaya masikini, mradi unaotekelezwa na TASAF awamu ya III.
Mnufaika wa Mpango wa kunusuru kaya masikini na mjasiriamali Elinita Mollel akiwa kwenye biashara yake ya kuuza nguo za mitumba, aliyoanzisha baada ya kupokea ruzuku ya TASAF.
Mnufaika wa Mpango wa kunusuru kaya masikini na mjasiriamali Riziki Naftali, akiwa kwenye biashara yake ya kuuza vyombo, aliyoanzisha baada ya kupokea ruzuku ya TASAF.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.