Friday 9th, May 2025
@Kituo cha Afya Nduruma
Wauguzi Halmashauri ya wilaya ya Arusha wanategemea kufanya maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani itakayofanyika tarehe 12.05.2018 kwenye viwanja vya Kituo cha Afya Nduruma.
Maadhimisho hayo yatatanguliwa na shughuli za utoaji huduma za afya 17 zitatolewa bure kuanzia kesho tarehe 09.05.28 mpaka siku ya kilele ya tarehe 12.05.2018.
Kwa siku hizo huduma zitatolewa kuanzia saa 02:00 asubuhi mpaka saa 12:00jioni.
Huduma zitakazotolewa ni pamoja na:-
1. Uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake.
2.Utoaji wa chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 14. 3. Upimaji wa Sukari na shinikizo la damu. 4. Upimaji wa VVU
5. Uchunguzi wa Fistula
6. Uchunguzi wa Kifua Kikuu TB.
7. Uchunguzi wa afya ya akili.
8. Uchunguzi wa macho
9. UChunguzi wa lishe
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.