Friday 9th, May 2025
@Ukumbi wa Mikutano Halmashauri ya Arusha
Mkurugenzi Mtendaji, anawatangazia wananchi wote kuhudhuria kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la kuwasilisha taarifa za Kata, mkutano utakaofanyika kesho tarehe 09.05.2018 kwenye Ukumbi wa Mikutano, halmashauri ya Arusha kuanzia saa 03:30 asubuhi.
Mkutano huo ni wa kawaida kwa mujibu wa sheria, ambao Waheshimiwa Madiwani wa kata zote 27, watapata fursa ya kuwasilisha taarifa za shughuli za maendeleleo zilizotekelezwa kwenye kata zao kwa kipindi cha robo ya tatu cha kuanzia mwezi Januari mpaka Machi 2018.
Hivyo wananchi wote wanaombwa kuhudhuria mkutano huo kwa ajili ya kusikiliza mwenendo wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika halmashauri yenu.
TUNATEKELEZA.......
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.