Friday 1st, December 2023
@UKUMBI WA MIKUTANO
TAARIFA KWA UMMA/VYOMBO VYA HABARI.
MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WA ROBO YA KWANZA 2O22/2023 TAREHE 04.11.2022
Halmashauri ya Arusha inategemea kufanya Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani (Full Council) wa robo ya kwanza mwaka wa fedha 2022/2023, kwa kipindi cha kuanzia Julai mpaka Septemba 2022. Mkutano huo utakaofanyika tarehe 04.11.2022 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo, kuanzia saa 03:00 asubuhi.
Mkutano huo wa baraza la Madiwani utakuwa na ajenda 10, huku agenda kuu zikiwa ni pamoja na Maswali ya papo kwa papo, Kujadili taarifa ya Mapato na Matumizi kwa mwezi Septemba 2022, Taarifa za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa robo ya kwanza, Kupitisha Mihtasari ya Kamati 4 za Kudumu za Halmashauri pamoja na kujadili Masuala ya kiutumishi.
Mkutano huo ni wa kawaida kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali za Mitaa. Mkutano Baraza la Madiwani ni Mkutano wa wazi, hivyo wananchi wote wa Halmashauri ya Arusha wanatakiwa kuhudhuria, ili kufuatilia kwa uwazi shughuli za utekelezaji wa Maendeleo zilizotekelezwa katika Halmashauri yao kwa kipindi cha miezi mitatu na robo ya kwanza, mwaka wa fedha 2022/2023.
Imetolewa na:-
Elinipa J. Lupembe.
AFISA MAWASISLIANO SERIKALINI
HALMASHAURI YA ARUSHA.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.