Friday 19th, April 2024
@VITUO VYOTE VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA
TAARIFA KWA UMMA/VYOMBO VYA HABARI.
CHANJO YA POLIO AWAMU YA NNE KWA WATOTO WA MIAKA 0 - 5
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, anapenda kuutarifu Umma kuwa Halmashauri itaanza rasmi zoezi la Kitaifa la kutoa CHANJO DHIDI YA UGONJWA WA POLIO kwa watoto wa kuanzia miaka 0 – 5, zoezi litakalofanyika kwa muda wa siku nne kuanzia tarehe 01- 04 Desemba, 2022.
Chanjo hiyo ya matone itatolewa kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali na vya binafsi hivyo wazazi/walezi wenye watoto wa umri huo, wanahimizwa kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo ya Polio kwenye vituo vilivyo karibu na maeneo wanayoishi.
Aidha Mkurugenzi Msumi amebainisha kuwa kutakuwa na huduma maalum ya Mkoba (Mobile Clinick) kwenye maeneo ambayo yako mbali na vituo vya afya na baadhi ya maeneo chanjo itatolewa kwenye Ofisi za Kata/Vijiji kulingana na taratibu zilivyopangwa na Idara ya Afya.
Wazazi/walezi wote mnatakiwa kuwapeleka watoto kupata chanjo hiyo muhimu inayowakinga watoto dhidi ya ugonjwa huo hatari wa Polio, ugonjwa ambao husababisha udumavu na ulemavu wa viungo hasa kwa watoto.
KINGA NI BORA KULIKO TIBA!!!!
Elinipa Lupembe
KAIMU MKUU WA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
30.11.2022
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.