Friday 9th, May 2025
@Arusha DC
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha anapenda kuwatangazia waombaji wote walioomba kazi ya Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II na Katibu Mahsusi Daraja la III kuwa usaili utafanyika tarehe 26 na 27 Juni, 2020 saa 2:30 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.
Aidha usailli wa mchujo (Written Interview) utafanyika tarehe 26/06/2020 na wasailiwa watakaofaulu ndio watakaochaguliwa kuendelea na Usaili wa Mahojiano (Oral Interview) tarehe 26/06/2020 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha siku ya tarehe 27/06/2020 kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Orodha ya waombaji walioitwa kwenye usaili ni kama inavyoonekana hapo chini, kwa waombaji ambao majina yao hayakuonekana katika orodha hiyo watambue kuwa maombi yao hayajakidhi sifa kwa mujibu wa nafasi zilizotangazwa. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha anawashukuru kwa kuleta maombi ya kazi na wasisite kutuma tena maombi kipindi Halmashauri itakapotangaza nafasi za kazi ambazo zitaendana na sifa walizonazo.
Waombaji wote walioitwa kwenye Usaili wanatakiwa kuzingatia maelekezo yafuatayo:
ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.