• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

ARUSHA DC yaendelea kuboresha miundombinu ya madarasa kwa ufadhili wa Ubalozi wa Japani

Posted on: July 5th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Katika kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa unaozikabili shule nyingi nchini, unaosababishwa na ongezeko la wanafunzi wanaodahiliwa shuleni, katika awamu hii ya tano, kutokana na Serikali kutekeleza elimu bila malipo.

Halmashauri ya Arusha imeendelea kutekeleza miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule zake, kwa kushirikiana na wadau  mbalimbali wa maendeleo, wa ndani na nje ya nchi, ili kukabiliana na upungufu huo.

Shule ya sekondari ya Sokon II kata ya Sokon II, ni miongoni mwa shule za  Sekondari, Halmashauri ya Arusha, ambayo imepata neema ya pekee ya kujengewa vyumba vinne vya madarasa na vyoo, kwa ufadhili wa Ubalozi wa Japani nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha Dkt. Wilson Mahera ameeleza kuwa, ubalozi wa Japani umetoa kiasi cha shilingi milioni 196.2, kwa ajili ya kukamilisha, ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, vyoo vya wanafunzi, pamoja na samani za madarasa hayo pindi ujenzi huo utakapokamilika.

Aidha, Dkt. Mahera amefafanua kuwa, kiasi hicho cha fedha kitatumika, kujenga msingi wa jengo la ghorofa la sakafu tatu, na kukamilisha  vyumba hivyo vinne vya madarasa, huku kila sakafu ikitarajiwa kuwa na vyumba vinne na vyoo vya wanafunzi, na kufanya jengo hilo lote, kuwa na jumla ya vyumba 12 pindi litakapokamilika.

"Kutokana na uhaba wa ardhi, jengo hilo litakuwa la ghorofa, na kiasi hicho cha fedha, kitatumika kujenga msingi  wa ghorofa hilo, na kukamilisha vyumba vinne vya madarasa na vyoo vya wanafunzi pamoja na meza na viti vya wanafunzi"  amethibitisha mkurugenzi Mahera

Naye Mkuu wa shule ya Sekondari Sokon II,mwalimu Mwamvita Kilonzo, amesema kuwa, kukamilika kwa vyumba hivyo vya madarasa, kutapunguza msongamano wa wanafunzi darasani kwa asilimia 36% kutoka upungufu wa vyumba 11 vya madarasa uliokuwepo.

Ameongeza kuwa, Vyumba hivyo vya madarasa vinategemewa kusomea jumla ya wanafunzi 189 kwa uwiano wa wanafunzi 45 kwa darasa moja, na kutasaidia kuwa na mazingira rafiki  kwa walimu na wanafunzi ya kuwezesha kitendo cha kufundisha na kujifunza kuwa rahisi.

Awali, Shule ya sekondari Sokon II ina jumla ya Wanafunzi 1,013, kutokana na idadi hiyo ya wanafunzi, shule hiyo ilikuwa na upungufu wa  vyumba 11 vya madarasa, na baada ya kukamilika vyumba hivyo 4, kutakuwa na upungufu wa vyumba 7 ambayo tayari kuna mikakati ya ujenzi wa vyumba hivyo. 

Halmashauri ya Arusha inatekeleza kwa vitendo, mikakati na Sera za serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoahidi watanzania kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi, wakati wa Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.







Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.