Leo, tarehe 6 Septemba 2025, Shule ya Msingi Sekei imefanya mahafali ya darasa la saba ambapo wanafunzi waliokuwa wakihitimu wameaga rasmi ngazi ya elimu ya msingi. Hafla hiyo ilihudhuriwa na walimu, wazazi na wageni mbalimbali waalikwa, huku ikipambwa na burudani, hotuba na pongezi kwa wahitimu.
Katika tukio hilo, wanafunzi walihimizwa kuendelea kuwa na nidhamu, bidii na ujasiri wanapoanza safari mpya kuelekea ndoto zao kubwa za kielimu na kimaisha. Mahafali haya yameacha alama ya kumbukumbu muhimu kwa shule na jamii ya Sekei kwa ujumla.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.