Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Ndugu Seleman H. Msumi na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Meru Bi. Zainabu Makwinya wameungana na viongozi na wadau mbalimbali katika Mkutano wa 4 wa Wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na Ujifunzaji (MEL) unaofanyika katika Ukumbi wa Malaika Resort jijini Mwanza.
Mkutano huo ni jukwaa muhimu linalowawezesha wataalamu, watunga sera, watafiti na watekelezaji kubadilishana maarifa na mbinu bora za kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na tathmini nchini.
ambapo Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu (PMO-PPC) kwa lengo la kuimarisha umiliki wa ndani wa mifumo ya MEL na kujenga mazingira endelevu ya tathmini. Aidha, unalenga kuongeza uelewa na mshikamano katika kukuza matumizi ya ushahidi katika uundaji sera na utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Kwa upande wake, Ndugu Seleman H. Msumi na Mwl. Zainabu Makwinya wameshiriki kama wawakilishi wa Halmashauri zao ili kutoa mchango wa uzoefu na kuimarisha mifumo ya uwajibikaji katika ngazi za halmashauri. Ushiriki wao unatarajiwa kuchochea mbinu shirikishi na endelevu katika ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo ya wananchi.
Mkutano wa 4 wa Wiki ya MEL unasisitiza ajenda kuu tatu: kuimarisha mifumo ya MEL katika ngazi za kijamii, kikanda na kitaifa, kukuza matumizi ya ushahidi katika uundaji sera na utoaji huduma bora, pamoja na kuhamasisha ushirikiano katika ufadhili na maendeleo ya taasisi zinazojihusisha na MEL.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.