Na Elinipa Lupembe
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, wilaya ya kichama Arumeru Komredi Noel Severe, amekiri kuridhishwa na utekelezaji wa Ilani ya chama hicho, halmashauri ya Arusha
Mwenyekiti huyo amekiri hayo wakati wa uzinduzi wa jengo la maabara ya Masomo ya Sayansi shule ya sekondari Oldonyowas, mradi uliotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF.
Komredi Severe ameweka wazi kuwa, serikali yaawamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kisekta katika halmashaui ya Arusha, serikali ikiwa na mategemeo makubwa ya matokeo ya miradi hiyo kwa wananchi.
Aidha Mwenyekiti huyo ameweka wazi kurishishwa na utekelezaji wa mirai yenye kuzingatia viwango vya ubora unaoendana na tahamani halisi ya fedha zinazotolewa na serikali, ikiwa ni utekelezaji wa Ilana ya CCM ya 2020
"Ninapongeza kazi nzuri mnazozifanya na watalamu katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, miradi ni mizuri inayozingatia viwango vya ubora kulingana na thamani ya fedha 'value for money' na kutoa matokeo chanya ya utoaji na upatikanaji wa huduma kwa wananchi, hii nidhahiri tunamuunga mkono Mhe. Rais, katika utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020, ninawapongeza sana watalam na wananchi kwa ujumla"Ametoa pongezi hizo
Hakusita pia kuwapongeza wananchi kwa ushiriki wao katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kwa kujitolea nguvu kazi kwenye shughuli za ujenzi, pamoja na usimamizi wa miradi inayotumia 'force akaunti' huku mafundi wazawa wakijitoa kwa hali na mali kutekeleza miradi hiyo bila kujali kiasi cha pesa wanachokipata
Hata hivyo amewasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii, kwa kuwa lengo la serikali inayoongozwa na CCM ni kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu ya msingi kuanzia darasa la awali mpaka kidato cha nne bila malipo na katika maeneo karibu na nyumbani, na tayari serikali imekwisha tekeleza jukumu hilo.
Ameongeza kuwa hapo awali jamii za kimaasai watoto wa kike hawakupata fursa ya kupata elimu ya sekondari, kutokana na mila na desturi lakini pia uchache wa shule kwa wakati huo, ameongeza kuwa kwa sasa serikali imejenga shule za sekondari kila kata, zilizotoa fursa kila mtoto kupata nafasi ya masomo ya sekondari.
"Niwatie moyo wasichana, someni kwa bidii, wanawake mnaweza, hakikisheni mnatumia fursa hii adhimu, someni kwa bidii sana, na kufikia ndoto zenu, tunatarajia kupata watalamu wa fani mbalimbali hapa na viongozi wengi wa ngazi tofauti". Amesisitiza Mwenyekiti huyo wa CCM.
Mradi wa ujenzi wa jengo la maabara mbili za somo la Fizikia na Jiografia, umetekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 99.7 fedha kutoka serikali Kuu kupitia Mfuko wa Maendelei ya Jamii TASAF.
Ikumbukwe kuwa uboreshaji wa miundombinu ya shule na ujenzi wa maabara ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2022 sura ya tatu, Ibara ya 80, Kifungu (a)Kujenga na kukarabati miundombinu ya elimu pamoja na kuhifadhi na kuendeleza mazingira ya shule hizo; kifungu na kkifung (d)Kuimarisha ufundishaji wa masomo ya sayansi yakiwemo Hisabati,Fizikia, Kemia na Baiolojia na kkuongeza upatikanaji wa walimu wa kufundisha masomo hayo.
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.