Na Elinipa Lupembe
Watanzania wilayani Arumeru, wamekumbushwa kuhakikisha kwa nguvu zote wanailinda, wanaitunza na kuipambania amani ya nchi hii kwa kuwa ni tunu iliyoachwa na mashujaa wazalendo wa taifa.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatigikolo Kaganda, wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa kiwilaya, yaliyofanyika eneo la USA River huku akiwasisitiza wanaarumeru kulinda amani ambayo ndio tunu ya Taifa, tunu ambayo ni urithi ulioachwa na vizazi vilivyotangulia.
Mkuu huyo wa wilaya ameweka wazi kuwa katika kumbukumbu ya siku muhimu ya Mashuja ni jukumu la kila mmoja kufahamu kuwa amani, upendo na utulivu unaotawala nchini, ni urithi uliochwa na mashujaa waliojitoa kizalendo kulipigania Taifa hili huku wengine wakipoteza maisha yao wakati wakiilinda na kuipigania amani ya nchi yao.
"Tunapofanya kumbukumbu ya siku hii muhimu, tuwaenzi Mashujaa wetu kwa kulinda tunu ya amani ya nchi yetu, wapo waliopoteza maisha kwa ajili ya Taifa hili, amani hii tuithamini na kuilinda kwa nguvu zote kama yai ili lisivunjike, tudumishe amani, upendo na mshikamano wa nchi yetu bila kujali tofauti za itikadi zetu" Amesisitiza Mkuu huyo wa wilaya.
Aidha amewataka watanzania kila mmoja kwa nafasi yake, kuendelea kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kwa bidii ili kusukuma gurudumu la maendeleo la nchi na kuongeza kuwa kasi ya amendeleo ya serikali ya awamu ya sita, iwape ari ya kufanyakazi kwa bidii.
Amewawasistiza vijana ambao ndio nguzo ya maendeleo ya Taifa, kuwa wazalendo wa nchi yao kwa kujikita kwenye shughuli za uzalishaji mali zaidi kwa kuwa wao ndio nguvu kazi ya Taifa na kuwapuuza watu wanaowapotosha na kuwashawishi kujiingiza kwenye vitendo vibaya ambavyo ni kinyume na maadili yanayokinzana na mila na desturi za jamii zetu.
Hata hivyo wananchi wa wilaya ya Arumeru, waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku hiyo muhimu ya Mashujaa, wameipongeza serikali ya awamu ya sita, chini ya mama Samia Suluhu Hassan kwa kasi ya maendeleo katika sekta zote, kasi ambayo inawafanya wananchi kuendelea kuwa na amani na utulivu huku kila mmoja akijikita kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Mzee Emmanuel Kaaya amebainisha kuwa, kasi ya maendeleo inayofanywa na mama Samia, inawafanya watanzania kujikita kwenye shughuli za uzalishaji mali zaidi jambo ambalo linaendelea kudumisha amani na mshikamano wa Taifa.
"Serikali ya awamu ya sita imefanya mapinduzi makubwa ya kimaendeleo, kwenye elimu, afya, maji na hata miundombinu ya barabara, wananchi tunapata huduma nyingi za kijamii kirahisi na zinaoatikana maeneo jirani sasa, jambo hili linatupa amani, upendo na utulivu wa kuendelea kulijenga Taifa letu" Amesema Anna Sinai mkazi wa Usa River.
Awali mkuu wa wilaya ya Arumeru amewaongoza wakazi wa wilaya hiyo kuadhimisha siku ya Mashujaa kwa kupanda mito kwenye mto Ndurumanga, pamoja na kufanya usafi wa mazingira kwenye eneo la Leganga na kituoc ha Afya cha Usa River.
ARUSHA DC NI YETU, TUSHIRIKIANE KUIJENGA
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.