Na. Elinipa Lupembe.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, amewaagiza viongozi na wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa ya Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa wa Mapambano dhidi yaUVIKO 19, halmashauri ya Arusha, kuongseza kasi ya uengenezaji wa viti na meza na kukamilisha ifijapo tarehe 20.12.2021.
Mkuu huyo wa wilaya, ametoa rai hiyo, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika halmashauri hiyo, na kiweka wazi kuwa, shughuli za ujenzi ziko kwenye hatua za ukamilishaji lakini bado kazi ya utengenezaji wa viti na madawati inahitaji kuongeza kasi.
"Nimeridhishwa na hali ya maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa lakini zinahitajika jitihada za ziada kukamilisha utengenezaji wa samani za madarasa hayo, ongezeni kasi ya kutengeneza viti na meza, mafundi watengeneze usiku na mchana ili darasa likamilike likiwa na samani zake, kama yalivyo maelekezo ya serikali" amesisistiza Mhandisi Ruyango
Hata hivyo wakuu wa shule, wameahidi kuwasimamia mafundi, kutengeneza samani hizo, usiku na mchana ili kuhakikisha zinakamilika kwa muda uliopangwa, licha ya kuwa na chamgamoto ya kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya siku.Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa wilaya ametembelea shule sekondari Bangata yenye madarasa 2, shule ya sekondari Ilkiding'a inayojenga madarasa 11, shule ya sekondari Kiranyi, inayojenga madarasa 13, shule ya sekondari Mringa inayojenga madarasa 10 na shule ya sekondari Matevesi inayojenga madarasa 3.
Ikumbukwe kuwa kutokana na changamaoto mbalimbali za ukamilishaji ujenzi huo, serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, imeongeza muda wa kukamisha ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa mpaka kufikia tarehe 31, Desemba 2021 badala ya tarehe 15. Desemba 2021 kama ilivyokiwa hapo awali.
Awali, Halmashauri ya Arusha inajenga jumla ya vyumba 100 vya madarasa na madawati, huku madarasa 96 shule za sekondari na madarasa 4 shule mbili za msingi shikizi, kwa gharama ya shilingi bilioni 2, fedha za Mpango wa Maendeleo na Ustawi wa Taifa wa Mapambano dhidi ya UVIKO 19.
ARUSHA DC
#KaziInaendelea✍✍
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango (aliyevaa kofia) akikagua baadhi ya madawati yanayotengenezwa kwenye karakana ya shule ya sekondari Mringa, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa ya mpango wa maendeleo na ustawi wa Taifa wa Mapambano dhidi ya UVIKO 19, katika halmasahuri ya Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango (aliyevaa kofia) akikagua maemdeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa 4 lenye vyumba 13 vya madarasa shule ya sekondari Kiranyi, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa ya mpango wa maendeleo na ustawi wa Taifa wa Mapambano dhidi ya UVIKO 19, katika halmasahuri ya Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango (aliyevaa kofia) akikagua maemdeleo ya ujenzi wa jengo la ghorofa 4 lenye vyumba 13 vya madarasa shule ya sekondari Kiranyi, wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba 100 vya madarasa ya mpango wa maendeleo na ustawi wa Taifa wa Mapambano dhidi ya UVIKO 19, katika halmasahuri ya Arusha
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.