MHE. KAGANDA AMEONGOZA ZOEZI LA USAFI NGARAMTONI
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama leo Mei 25, 2024 ameongoza zoezi la usafi Ngaramtoni kata ya Olmotonyi pamoja na wananchi wa maeneo hayo
Mhe. Kaganda ametoa rai kwa wananchi wa Wilaya ya Arumeru kuenzi utamaduni wa kufanya usafi kila ifikapo Mwisho wa Mwezi kwani ni agizo la kitaifa kupitia Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, Mhe. Kaganda amewataka wananchi kulinda maeneo yao ili kuwa safi na kumtaka Mkurugenzi kupitia idara za Mazingira kutoza faini wote wanaochafua mazingira na kuwataka wanachi kuweka utaratibu mzuri wa kutunza mazingira yao.
Katika Hatua nyingine Diwani wa viti Maalumu FARAJA EMANNUEL amemwomba Mkuu wa Wilaya zoezi hili liwe angalau mara mbili kwa mwezi tarehe 15 na tarehe 30 wakati Wilaya ikiendelea kujipambambanua kuweka maeneo safi hadi pale maeneo yatakapokuwa yanaridhisha ndio iwe mara moja
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kichama Arumeru LEMPAMPA LUKUMAY ameishukuru Serikali na kuahidi kuendelea kuwa balozi wa mazingira na kuwawajibisha wale wote watakaojaribu kuchafua mazingira.
Halikadhalika, Waendesha bodaboda nao wameipongeze Serikali kwa hatua wanayoichukua dhidi ya Mazingira James Paul Miongoni mwa Madereva bodaboda amekiri kuwa ni kweli mazingira yao yanapokuwa safi inawavutia pia wateja kuweza kufanya kazi nao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.