DC ARUMERU ATATUA MGOGORO WA MFEREJI WA MAJI KATI YA KIJIJI CHA MAJIMOTO NA WAMILIKI WA SHAMBA LA GOMBA ESTATE
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda ametatua mgogoro wa mfereji wa maji kati ya katika Kijiji cha Majimoto, kata ya Nduruma na Wamiliki wa shamba la Gomba Estate, mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka mitatu bila utatuzi.
Mgogoro huo ulikuwa unahusisha uongozi wa shamba la Gomba Estate kuzuia mfereji wa maji kupita katika shamba hilo kuelekea kwenye Kijiji cha Majimoto, mfereji ambao hutumika kwa shughuli za kilimo, hali iliyosababisha mazao ya wananchi hao kunyauka na kukosa mavuno kwa kipindi chote hicho.
Akizungumza na wananchi wa pande zote mbili kwa nyakati tofauti, Mhe. Emmanuela ameuagiza uongozi wa shamba hilo kuruhusu njia ya maji kupita katika shamba ili wananchi wa Majimoto waweze kupata maji na kunusuru mazao ya wananchi hao ambayo yananyauka shambani kutokana na ukame unaoendelea katika Kijiji hicho.
“Kaeni viongozi wa pande zote na kuweka kuweke utaratibu mzuri ili watu wote mpate maji kwa zamu, hairuhusiwi mtu yoyoyote kizuia maji kwa maslahi yake binafsi, utaratibu wa zamu, utaratibu utakaowezesha kila upande kunufaika mtakao uweka kwa kuzingatia taratibu za Mamlaka ya Bonde la Mto Pangani wameshaweka utaratibu na kutoa kibali cha kutumia maji haya”. Amesisitiza Mkuu huyo wa Wilaya.
Hata hivyo, utatuzi huo umekuja baada ya wananchi wa Kijiji hicho cha Majimoto kutaka majibu kutoka kwa Serikali kuhusu mgogoro huo huku wakidai wamechoshwa na kero ya mazao yao kuharibika mashambani kwa kukosa maji ya uhakika na kusababisha kukumbwa na baa la njaa kwa kipindi chote hicho.
“Tunaamini viongozi wetu wanaohusika na maji wanafanya kazi zao vizuri, lakini huyu msimamizi wa shamba la Gomba Estate amekuwa chanzo cha mazao ya wanakijiji hiki kuungua kila mwaka”. Alisema mmoja wa wanakijiji hao, Yohana Ming’arana wakati akiwasilisha kero hiyo kwa Mkuu wa Wilaya.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumia maji Bonde la Mto Nduruma, Mariaki Mollel ameahidi kuendelea kusimamia mgao wa maji hayo ipasavyo ili wananchi wote wa Kijiji hicho waweze kunufaika kwani hiyo ni Rasilimali ya Taifa na hakuna mwananchi yeyote mwenye umiliki wa maji huku akisisitiza upendo baina ya wanakijiji hao.
Awali wananchi wa kijiji cha cha Majimoto kata ya Nduruma kupitia Jumuia ya watumia maji, na Uongozi wa shamba la Gomba Estate waliingia kwenye mgogoro baada ya uongozi wa shamba hilo kuzuia mfereji wa maji kupita kwenye eneo la shamba la Gomba Estate.
"ARUSHA DC Ni Yetu, Tushiikiane Kuijenga"
#KaziIendelee
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.