Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emanuela Kaganda ameongozana na Mwenyekiti wa CCM wiliaya ya Arumeru Noah Severe kuwatembelea wahanga wa mvua kubwa maeneo ya kata ya Oloirineni.
Mhe. Kaganda amesema kuwa licha ya kuwa hakuna taarifa za mvua hizo kusababisha vifo lakini madhara yaliyotokana na mvua hiyo yamesababisha hasara kubwa huku familia moja ikikosa makazi.
Naye Mwenyekiti wa CCM Severe, ametoa pole kwa wahanga wote wa mvua hizo na kuwataka wananchi kuwasaidia wahanga kwa hali na mali pamoja kuendelea kuchukua tahadhali ya mvua zijazo.
Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya ya Arumeru aliambatana na Kamati ya ulinzi na Usalama pamoja na Kamati ya Siasa wilaya ya Erumeru ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Arumeru.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.