Na. Elinipa Lupembe
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mhe. Jerry Muro, amefanya ziara kwenye kijiji cha Engutukoit kata ya Oldonyowas, halmashauri ya Arusha na kukagua miundombinu ya Mabwawa ya maji kwa ajili ya mifugo.
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kuyatunza mabwawa hayo kwa ajili ya kunyweshea mifugo yao wakati wa kipindi cha kiangazi,ili mifugo yao iweze kupata afya na wafugaji hao kufanya mifugo biashara kuelekea uchumi wa viwanda.
Ameongeza kuwa uwepo wa chakula cha kutosha cha mifugo ikiwemo maji, kutawezesha mifugo hiyo kuwa na afya bora, na kuwa na zao bora la mifugo litakalowezesha wafugaji kujiongezea kipato.
"Nimeona ni busara kufanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya mifugo ya wananchi wetu haswa wa jamii ya kifugaji Halmashauri ya Arusha, nimetembelea na kukagua mabwawa mawili katika kijiji cha Engutukoiti kata ya oldonyowasi sisi kwetu tunajiandaa kabla ya kiangazi, uongozi ni kujipanga ma kuona mbali na kujiandaa na yajayo
Hata hivyo wananchi wa Engutukoit licha ya kumshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa kuwatembelea, wameahidi kutunza mabwawa hayo, ili kuwa na uzalishaji wa mifugo bora kwa ajili ya ustawi wa vipato vya familia zao.
#2020Kazikwetu #WafugajiWetu #ArumeruYetu
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.