Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, amewataka wanawake kuhakikisha wanafanya miradi waliyokusudia ili kuweza kurejesha fedha hizo kwa wakati ili fedha hizo ziweze kuwanufaisha na wengine.
Mkuu huyo wa wilaya amesema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi mkopo wa shilingi milioni 274 kwa vikundi 37 vya wanawake na vijana, hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya makao makuu ya halmashauri ya Arusha.
Mheshimiwa Emmanuela amewasiistiza wanavikundi hao kutambua fedha hizo zinatakiwa kurejeshwa baada tu ya kipindi cha neema, hivyo ni vema kutumia fedha hizo kwa kufanya miradi waliyoiandika kwenye maandiko yao na kuweza kurejesha kwa wakati.
"Tukirejesha fedha hizi kwa wakati tutatoa fursa ya kuwakopesha wengine na sisi wenyewe kukopeshwa kwa awamu nyingine, tumieni fedha hizi kwa nidhamu" Amesisitiza Mkuu huyo wa wilaya
Aidha amewasisitiza wanawake kuwahamasisha na kuwaelimsiha vijana ili waweze kunufaika na mikopo isiyo na riba inayotolewa na serikali kupotia asilimi 10 za mapato ya ndani ya halmashauri
"Kina mama tunalo jukumu la kuwaelimisha vijana wetu ili nao wajitokeze kwa wingi kuchukua mikopo hii, leo tunatoa mikopo lakini vikundi vya vijana ni viwili tu, ninaamini mikono ya kina mama inalea, waleeni vijana, wajengeeni uweo wa kufanya kazi kama ninyi ili wanufaike na fursa hii adhimu". Amesisitiza Mhe. Mkuu wa wilaya.
Hata hivyo wanavikundi waliopokea mikopo hiyo wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwapa fursa inayowawezesha kujikwamua kiuchumi, kupitia mikopo hiyo isiyo na riba.
Habibu Malia kijana mwenye ulemavu, amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu kwa mpango huo wa kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi na kuwasihi vijana kujitokeza kutumia fursa hiyo, kwa kuwa ni kweli inapatikana.
"Tunaishukuru serikali yetu kwa kutupa mikopo hii yenye masharti nafuu, hata sisi vijana wa kijijini kabisa tumeweza kukopesheka, jambo ambalo halipatikani kwenye taasisi nyingine za kifedha". Amesema Joseph Mibaroi wa kikundi cha KIDALI Youth Group cha kata ya Mwandeti.
Akizungumza kabla ya kukabidhi mikopo hiyo, mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 3 halmashauri imefanikiwa kutoa mikopo ya shilingi bilioni 1.3 na kwa kipindi cha miezi sita ya mwaka wa fedha 2022/23 imekopesha shilingi milioni 509.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arumeru, Noel Severe ameipongeza halmashauri kwa kutekeleza Ilani ya chama ya mwaka 2020 - 2025 ya kupambana na umaskini kwa kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuwapa mikopo isiyokuwa na riba.
"Mikopo hii ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, hivyo mnapaswa kuhakikisha mnaitumia vizuri iweze kuinua vipato vya familia pamoja na tunategemea mkapambane na kurejesha kwa wakati,,kulingana na utaratibu". Amesema Mwenyekiti wa CCM
Awali mkuu wa wilaya ya Arumeru amekabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 274 kwa vikundi vya wanawake na vijana ikiwa ni 10% ya mapato ya ndani kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
KaziIendelee
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.