Na Elinipa Lupembe
Walimu wametakiwa kufanyakazi kwa weledi kwa kuzingatia miongozo wa elimu, iliyotolewa na serikali yenye lengo la kuimarisha utoaji wa elimu nchini na uimarishaji hali ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango, wakati akizindua miongozo wa elimu katika halmashauri ya Arusha, zoezi lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Mkuu huyo wa wilaya ameelezea kuwa, wanufaika wakubwa wa mwongozo huo ni wanafunzi hivyo ni vyema viongozi wa ngazi zote kusimamia utekelezaji wake, na kuwasisitiza walimu kuitendea haki miongozo hiyo, kwa kuwa wao ndio watekelezaji wakuu ili kumfikia mlaji ambaye ni mwanafunzi.
"Serikali inategemea matokeo chanya ya miongozo hii, na walimu ndio watekelezaji wakuu kwa kuifanyia kazi moja kwa moja kwa wanafunzi ambao ndio walengwa, hivyo tunawategemea ninyi walimu, mnapaswa kufanya kazi kwa weledi ili kufikia malengo ya serikali". Amesisitiza Mhandisi Ruyango.
Mwongozo unaekekeza kuandikisha wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza kuanzia mwezi Oktoba na huu ndio msimu, anzeni kuandikisha watoto sasa, kusiwe na mtoto mwenye umri wa kuandikishwa shule anaachwa, mpaka kufikia mwezi ....wote wawe wameandikishwa.
Nao wanafunzi, walioshuhudia uzinduzi huo, wameipongeza serikali kwa kuandaa miongozo hiyo, na kuthibitisha kuwa miongozo yote inamanufaa makubwa kwao, huku wakiamini serikali ina mipango thabiti kwa wanafunzi na kuinua kiwango cha taaluma nchini.
"Ninaipongeza serikali kwa miongozo hii ambayo dira yake inaelekeza wanufaika wakuu ni sisi wanafunzi, tunamshukuru mkuu wetu wa wilaya, tunamshukuru Rais wetu, mama Samia Suluhu Hassan, kwa kuimarisha mpango wa elimu nchini, unaotunufaisha sisi wanafunzi" Amebainisha Joshua Lenatus, mwanafunzi wa darasa la 5, shule ya msingi Sekei.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameahidi kusimamia utekelezaji wa mwongozo huo kwa shule zote, kwa kushirikana na timu nzima ya elimu, na kuhakikisha mwongozo huo unazaa matunda yaliyokusudiwa na kufikia lengo la serikali.
Awali mwongozo wa elimu nchini umejikita katika namna ya uteuzi wa viongozi wa elimu, mkakati wa kuimarisha ujifunzaji na ufundisha unaotumia zana halisi na wanafunzi kumudu stadi za kusoma kuandika na kuhesabu, utatuzi wa changamoto katika uboreshaji elimu ya msingi na sekondari pamoja na mwongozo wa utoaji huduma za chakula na lishe shuleni.
ARUSHA DC
Tupo kazini ✍✍✍
PICHA ZA MATUKIO
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, akikata utepe kitabu cha miongozo ya Elimu, kama ishara ya kuzindua miongozo hiyo katika halmashauri ya Arusha, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, akiwakabidhi kitabu cha miongozo ya Elimu, Afisa Elimu na Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiutu, mara baada ya uzinduzi wa miongo hiyo katika halmashauri ya Arusha, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango, akiwakabidhi kitabu cha miongozo ya Elimu, Afisa Elimu na Afisa Mtendaji wa Kata ya Oloirin, mara baada ya uzinduzi wa miongo hiyo katika halmashauri ya Arusha, hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa miongozo ya Elimu katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha
Baadhi ya Maafisa Elimu Kata waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa miongozo ya Elimu katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango na wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa miongozo ya Elimu katika ukumbi wa mikutano halmashauri ya Arusha
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.