Na Elinipa Lupembe
Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha Seleman Msumi, amewaongoza wanafunzi wa shule za Msingi Olkokola na Engorika kata ya Lemanyata, katika zoezi la upandaji miti ikiwa ni muendelezo wa Kampeni ya upandaji miti, halmashauri ya Arusha mwaka 2023.
Katika zoezi hili Mkurugenzi Msumi, amewataka wanafunzi hao kuhakikisha kila mmoja anautunza mti wake alioupanda mpaka atakapoondoka shuleni hapo.
Amewasisitiza wanafunzi wote kupanda miti shuleni na nyumbani pia ili kuhifanyi uoto wa asili katika maeneo yao, ikiwa ni mapambano ya kukabiliana na ukame unaoikabili nchi yetu na dunia kwa ujumla wake.
Aidha amewataka walimu na wazazi kuwasimamia watoto kupanda mti shuleni na nyumbani na kuhakikisha wanaitunza katika maisha ya kukua kwao.
Hata hivyo wanafunzi wa shule hizo, wamefurahishwa na zoezi la upandaji miti, zoezi ambalo wamekiri kuwapa matumaini ya maisha bora ya baadaye.
Unice Elias mwanafunzi wa darasa la sita, amekiri kupanda miti saba nyumbani na shule miti 3, miti ambayo ameahidi kuitunza miti hiyo.
"Nitawaelimisha wazazi wangu umuhimu wa kupanda miti na kuitunza, na kufungia mifugo ili isiharibu miti tuliyoipanda".Amesisitiza Caroline Lazaro
Mti wangu, Taifa langu, Mazingira yangu, KaziIendelee
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.