JE NI TAARIFA ZA AINA GANI ZITAKAZOKUSANYWA WAKATI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022?
Taarifa zitakazoulizwa na KARANI wa SENSA zitahusu:-
1. Majina Kamili ya Wanakaya (Majija matatu)
2.Taarifa za kidemografia (umri, jinsi, hali ya ndoa- ameoa/ameolewa).
3. Taarifa za ulemavu (aina ya ulemavu na chanzo cha ulemavu).
4. Taarifa za Uraia / Uhamiaji.
5. Namba ya Kitambulisho cha utaifa na uhai wa wazazi.
6. Taarifa za elimu.
7. Taarifa za shughuli za kiuchumi.
8. Taarifa za umiliki wa ardhi na TEHAMA.
9. Taarifa za hali ya uzazi.
10. Taarifa za vifo na vifo vitokanavyo na uzazi.
11. Taarifa za nyumba, hali ya umiliki wa nyumba, vifaa/ rasilimali na udhibiti wa Mazingira.
12. Taarifa za kilimo, mifugo, uvuvi na misitu.
13. Taarifa kuhusu mpago wa TASAF.
14. Taarifa za majengo/nyumba.
15.Anwani za makazi.
16. Taarifa za huduma za kijamii katika ngazi kitongoji/shehia na mtaa.
HAKIKISHA UMEHESABIWA, TOA USHIRIKIANO KWA KARANI WA SENSA.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.