Na. Elinipa Lupembe.
# Kuzitaka Taasisi na Mamlaka zinazohusika na Wafanyabiashara za OSHA, TBS na TFDA, kutoa taarifa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, wakati wanapotaka kufanya shughuli zao ndani ya wilaya, ili kushirikiana ofisi hiyo na kuondoa sintofahamu zinazojitokeza baina ya wafanya biashara na mamlaka hizo.
#Kushughulikia na kuona namna ya kuwapunguzia wafanyabiashara tozo, zinazotozwa na halmashauri na OSHA, tozo ambazo, zinaonekana kutozwa kwa huduma zinazofanana na kutafuta uwezekano wa kubakiza tozo moja kati ya hizo.
#Kufuatilia na kuzitafutia ufumbuzi tozo na ushuru, zinazotozwa na Mamlaka za TBS, OSHA na TFDA, ikiwezekana ziwekwa kwenye 'package' moja, ili kuwapunguzia wafanyabiashara mzigo wa tozo.
#Kuwaunganisha wafanya biashara wote wa Arumeru na Baraza la Biashara na kupata fursa ya kuwakutanisha na Wawekezaji na kutafuta masoko ya bidhaa zao.
#Wafanya biashara wamehimizwa, kushiriki, kwenye maonesho ya NANENANE 2019, kupitia mabanda ya Arusha DC na Meru DC, yaliyopo kwenye Viwanja vya NANENANE Njiro.
#Kukutana na kufanya Vikao na wafanyabiashara mara mbili kwa mwaka, na hatimaye kukubaliana kikao kijacho, kifanyike tarehe 30.11.2019.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.