• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Jamii imetakiwa kushiriki kikamilifu kutunza miundo mbinu ya maji pamoja na rasilimali maji

Posted on: March 4th, 2018

Jamii imetakiwa kushiriki kwa hali na mali kutunza rasilimali maji pamoja na kusimamia miundo mbinu ya maji inayojengwa kwenye maeneo yao ili miradi ya maji inayojengwa iwe endelevu kwa miaka mingi ijayo. 

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa Idara ya huduma za Jamii Idara ya Maendeleo ya Kimataifa Uingereza 'DFID', Bi. Getrude Mapunda alipokutana na viongozi wa jamii kutoka eneo linalotekelezwa mradi wa maji wa vijiji vitano ndani ya halmashauri ya Arusha maarufu kama mradi wa maji wa WaterAid unaofadhiliwa na DFID kwa gharama ya shilingi bilioni 4.5. 

Mapunda amekutana na viongozi hao ili kuthibitisha ushirikishwaji wa jamii katika utekelezaji wa mradi huo ambao tayari miundo mbinu yake imeanza kuchimbwa na unategemea kukamilika mwishoni mwa mwaka huu wa 2018.

Licha ya kuridhishwa na uelewa wa pamoja waliokuwa nao viongozi hao baada ya kujengewa uwezo juu ya mradi huo wa maji, Mapunda amewataka viongozi hao kuendelea kuweka mikakati thabiti ya utunzaji wa mazingira ambayo ndio chanzo kikuu cha upatikanaji wa rasilimali maji. 

Aidha amendelea kufafanua kuwa miradi ya maji inatumia gharama kubwa kujengwa hivyo jukumu kubwa la wananchi ni kuwa na mikakati thabiti ya kuitunza na kuiendeleza miradi hiyo ili iweze kutumika kwa miaka mingi ijayo na vizazi vijavyo. 

"Ili mradi wa mji uwe endelevu ni jukumu la jamii kutunza miundo mbinu ya maji ikiwemo kuchangi gharama za maji kwa ajili ya maintainance pamoja na kutunza mazingira ya uhifadhi wa maji" amesema Mapunda. 

Naye mhandisi wa maji mkoa w Arusha Mhandisi Makaidi amethibitisha hali halisi ya kupungua kwa kiasi cha maji inayotokana na mabadiliko ya tabia nchi na kusababisha maji kupungua na kupatikana kwenye kina kirefu kadiri siku zinavyokwenda tofauti na miaka ya nyuma. 

Amefafanua kuwa suala la utunzaji wa mazingira linapaswa kupewa kipaumbele na jamii nzima ili kuepuka madhara makubwa ya ukosefu wa maji yanayoweza kutokea kwa siku za baadaye. 

"Tafiti zinaonesha kwa sasa maji yanapatikana urefu wa mita 100 mpaka 150 kwenda chini, kama tusipochukua hatua madhubuti miaka kumi mpaka ishirini ijayo maji hayo yatapatikana kina cha mita 200 mpaka 300 jambo ambalo litaathiri hata miradi hii inayotekelezwa sasa" amesisitiza Mhandisi Makaidi. 

Hata hivyo viongozi wa jamii wa eneo la mradi wamethibitisha kuunga mkono juhudi za serikali za utunzaji wa mazingira, utunzaji wa miundo mbinu ya maji pamoja na uchangiaji wa gharama za huduma za maji ili kuendeleza miradi hiyo ya maji ambayo serikali na wafadhili hutumia gharama kubwa kuijenga. 

Wameongeza kuwa katika maeneo yao kumekuwa na agenda ya kudumu ya utunzaji wa mazingira kuanzia ngazi za familia na jamii nzima kwa kuhamasisha wananchi kutunza mazingira. 

Diwani wa kata ya Olkokola mheshimiwa Kalanga Laizer amesema kuwa wananchi wa kata yake wamehamasika kujenga vyoo bora baada ya kuwa na mkakati wa kutoza faini kwa nyumba isiyokuwa na choo bora na muitikio ni mkubwa kwa sasa. 

"Kwa sasa wananchi wa kwetu wana vyoo bora licha ya kuwa bado kuna changamoto ya maji katika maeneo hayo lakini tunaamini mradi huu ukikamilika shida itakwisha. Amesema Mheshimiwa Kalanga.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.