NA Elinipa Lupembe
Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango halmashauri ya Arusha, wanafanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha robo ya tatu ya Januari mpaka Machi 2023.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha, Mhe. Dkt. Ojung'u Salekwa, amesema kuwa wajumbe wa kamati ya Fedha wanakwenda kukagua miradi ya maendeleo ili kuona hali ya miradi na utekelezaji wake.
Ameongeza kuwa, Kamati hiyo ina wajibu wa kukagua na kubaini maendeleo ya miradi na kama kuna changamoto kujadili namna ya kuzitatua kwa wakati.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo, ametumia wasaa huo kuwapongeza wataalam wa halmashauri hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka kuendelea kushirikaina na wananchi, viongozi wa ngazi zote, kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa wakati kwa kuzingati vigezo vilivyowekwa na serikali.
Awali katika ziara hiyo, jumla ya Miradi 6 yenye thamani ya shilingi milioni 234.4, ikiwemo ujenzi wa nyumba ya mtumishi zahanati ya Ilkirevi, umaliziaji wa vyumba vitano vya madarasa na ofisi ya walimu, ukarabati wa kituo cha walimu - TRC Mringa, Kikundi cha vijana - KIDALI YOUTH GROUP, Ujenzi wa Zahanati kijiji cha Lemugur, ujezni wa uzio shule ya uzio wa shule ya msingi iliburu.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.