Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arumeru, Ndugu Noel Severe, amekagua utekelezaji wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Lemuguru, iliyojengwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF kwa gharama ya shilingi milioni 96 na unategemea kukakimila mwishoni mwa mwaka huu 2023.
Mwenyekiti huyo, ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, unaojidhihirisha thamani ya fedha kwa macho na kuwataka wananchi kuutunza mradi huo ili uweze kuwahudumia wananchi kama ilivyo malengo ya serikali
"Niwapongeze wanachi wa kijiji cha Lemuguru na uongozi wa kijiji na kata, kwa ushirikiano wao wa kushiriki katika utekelezaji wa mradi huo, hii imedhihirisha ushirikishwaji wa wanachi kwenye miradi ya maendeleo" Amefafanua Mwenyekiti Severe.
Naye Mwenyekiti wa CCM kata ya Mateves Asha Said, amethibitisha uwepo wa changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya, katika kijiji cha Lemugur wanachi walikiwa wanateseka sana.
Aidha ameishukuru serikali uwepo kwa miradi mingi inayotekelezwa katika kipindi kifupi cha serikali ya awamu ya sita, miradi ambayo imetatua changamoto nyingi ndani ya kata.
Diwani wa kata ya Mateves, licha ya kuishukuru serikali kwa kuelekeza mradi wa zahanati kijiji cha Lemuguru, zahanati ambayo itawahudumia wananchi wa eneo hilo, wanachi ambao walikosa huduma hiyo kwa miaka yote.
Hata hivyo Mhe. Diwani huyo, ameweka wazi kuwa eneo hilo, limetolewa na mwananchi wa Lemuguru lenye thamani ya shilingi milioni 30, kwa ajili ya uwepo wa zahanati, kumpongeza kwa uzalendo alionao kwa kujitolea ardhi yenye thamani kwa vizazi vijavyo.
Ikumbukwe kuwa ziara hiyo ni maalumu kwa ajili ya ufuatiliaji wa utekelzaji wa Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 -2025.
"Arusha Dc ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.