Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango , halmashauri ya Arusha imefanya ziara ya kukagua jumla ya miradi ya maendeleo saba yenye inayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia 800 kwenye sekata za Elimu na Afaya.
Ziara hiyo ni ya kawaida kwa mujibu wa sheria ya Kamati hiyo kukagua utekelezaji wa miradi ya maenedele kwa kila robo ya mwaka, na ziara hiyo ilikuwa ni ya kipindi cha robo ya tatu cha Januari -Machi, kwa mwaka wa fedha 2017/18, yenye lengo la kukagua na kujionea utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo katika maeneo vijiji na kata ndani ya halmashauri, Ziara hiyo hufuatilia miradi ambayo hupitishwa na baraza la waheshimiwa madiwani wa halmashauri hiyo.
Jumla ya miradi sita katika sekta ya Elimu na Afya imetembelea ikiwa ni pamoja na mradi wa ujenzi na upanuzi wa Kituo cha Afya Nduruma, umaliziaji wa kituo cha Afya Manyire, ukarabati wa maabara shule ya sekondari Oldonyosambu na Sambasha, ujenzi wa darasa shule ya msingi Sambasha, shule ya sekondari Sambasha na Ilkiding'a pamoja na ujenzi wa Zahanati ya Kivululu kata ya Olturoto.
Aidha katika majumuisho ya ziara, licha ya kuonekana utekelezaji bora wa miradi hiyo, Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha Mhe. Noah Lembris kwa niaba ya wajumbe wa kati hiyo ya Fedha, ameendelea kusistiza kwa watalamu na wananchi hasa wajumbe wa kamati za ujenzi katika kata na vijij pamoja na watalamu, kuendelea kujifunza zaidi katika matumiz ya 'Forced Account' kwa lengo la kuondoa changamo zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Hata hivyo wajumbe wa kamati hiyo kwa pamoja wameendele kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo huku wakiwapongeza wataalam na wananchi kwa kujitoa kwa hali na mali wakati wa utekelezaji wa miradi katika maeneo yao.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.