Na Elinipa Lupembe
Jamii imetakiwa kuithamini na kuilinda amani ya Tanzania kwa kuwa amani na utulivu uliopo haipatikanini katika mataifa mengine na mataifa mengi wanaitamani na kuitafuta bila mafanikio.
Rai hiyo imetolewa na Kaim Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru, na Afisa Tarafaa kata ya Mbuguni, Abdala Teni, wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya mashujaa, yaliyofanyika kwenye shule mpya ya sekondari Kiutu, halmashauri ya Arusha, wilaya ya Arumeru.
Kaimu Katibu Tawala huyo, ameitaka jamii, kutambua kuwa misingi ya amani iliyopo nchini, imejengwa kwa muda mrefu na mashujaa wazalendo wa nchi ya Tanzania, hivyo kila mtanzania ana jukumu la kuilinda tunu hii, ili iendelee kudumu vizazi hadi vizazi.
Kila mtanzania anapaswa kutambua kuwa, wapo mashujaa waliopambana na hata wengine kupoteza maisha kwa ajili ya kupambania ukombozi wa Taifa hili, wapo mashujaa walioingunisha Tanganyika na Zanzibar ambayo leo watanzania wanajivunia Muungano na kuongeza kuwa ili kuilinda amani hii ni lazima kuweka uzalendo mbele katika kuilinda amani ya nchi.
"Tunapowakumbuka mashujaa walioipigania na nchi yetu, kika mtanzania anapaswa kuiombea na kuilinda amani ya Taifa hili ili iendelee kudumu, tunapaswa kuulinda Muungano kwa nguvu zote, tusikubali kupoteza amani yetu kwa itikadi za dini, siasa wala makabila kwa kuwa wapo mashujaa walioijenga misingi imara ya amani na utulivu wa Taifa la Tanzania" Amesisitiza Teni.
Naye Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, ameeleza licha ya kuwa lengo la kumbukizi ya siku hiyo, ni kuwakumbuka mashujaa waliopambania ukombozi wa nchi yetu, lakini zaidi ni kuendelea kuyaenzi matunda ya kuipigania nchi hii kwa kudumisha amani, upendo na mshikamano.
"Serikali inatambua na kuthamini damu ya watanzania iliyomwagika kwa ajili ya ukombozi wa nchi ya Tanzani, ni vema watanzania kwa umoja wetu, kudumisha amani iliyopo bila kujali tofauti zetu za kidini, kisisasa wala makabila yetu, Tanzania ni moja " amesisitiza Msumi.
Hata hivyo katika maadhimisho hayo, kulihudhuriwa na mzee shujaa wa Tanzanzia, ambaye ni mwenyekiti wa CCM kata ya Kiutu, mzee Wilson Meiludie, ambaye alishiriki vita vya Kagera na Uganda, mwaka 1978-79, amewataka watanzania kudumisha amani kwa kuwa madhara ya vita ni makubwa kwa jamii, madhara ambayo huacha makovu makubwa kwenye mioyo ya wanadamu.
"Niwasihi ndugu zangu, msiombe vita katika nchi yetu, nimeishuhudia vita, ni kitu ambacho sio kizuri kutokea katika jamii, watu wasio na hatia hupoteza maisha, huku uchumi wa nchi husika ukiporomoka na ni vigumu sana kuirudisha amani iliyopotea kwa ajli ya vita, tuna mifano kwa nchi za jirani, kwa miaka mingi wanapambana kuiridusha amani bila mafanikio" amebainisha mzee Meiludie
Awali wananchi halmasahuri ya Arusha, wameungana na watanzania kuadhimisha kumbukumbu ya siku ya Mashujaa nchini kwa kufanya usafi wa mazingira pamoja na kuotesha miti katika shule mpya ya sekondari Kiutu kata ya Kiutu.
Maadhimisho ya kumbukumbu ya siku mashujaa, yamefanyika kitaifa jijini Dodoma na hufanyika tarehe 25 Julai kila mwaka.
ARUSHA DC
#KaziInaendelea
JIANDAE KUHESABIWA
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA SIKU YA MASHUJAA 2022
Kaim Katibu Tawala wa Wilaya ya Arumeru, na Afisa Tarafaa kata ya Mbuguni, Abdala Teni, akiotesha mti kwenye shule mpya ya sekondari Kiutu, ikiwa ni shughuli za maadhimisho ya Kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, akiotesha mti kwenye shule mpya ya sekondari Kiutu, ikiwa ni shughuli za maadhimisho ya Kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
Mmoja wa mashujaa wa Tanzania, Mzee Wilson Meiludie, aliyeshiriki vita ya Uganda na Kagera, akiotesha mti kwenye shule mpya ya sekondari Kiutu, ikiwa ni shughuli za maadhimisho ya Kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
Mwenyekiti Halmashauri ya Arusha Mhe. Ojung'u Salekwa, akiotesha mti kwenye shule mpya ya sekondari Kiutu, ikiwa ni shughuli za maadhimisho ya Kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.