Makatibu muhtasi serikalini wametakiwa kufanyakazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kutunza siri za nyaraka mbalimbali za serikali katika maeneo yao ya kazi wakati wa mafunzo ya siku tano yaliyofanyika kwenye ukumbi wa halmshauri ya Arusha wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Afisa Elimu Takwimu Halmashauri ya Arusha ndugu John Charles amefunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, amewataka makatibu muhtasi hao kufanyakazi kwa weledi kwa kuwa taaluma yao iko katika kutunza siri za serikali na za watumishi kwa ujumla.
Ameeleza kuwa taaluma yenu inahitaji weledi na hekima ya hali ya juu katika utunzaji wa siri ndio maana katika serikali kuna masijala bayana ambayo ni ya wazi na masijala ya siri ambayo ninyi peke yenu ndio wahusika wa kutunza nyaraka hizo, hivyo ni vyema mkawa na tabia ya kujizuia kutoa siri kabla ya wakati wa kuweka jambo wazi.
Naye mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya Muda Mfupi kutka chuo cha Utumishi wa Umma Tabora ndugu Musa Ligembe amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watumishi hao juu ya utunzaji wa nyaraka za siri za serikalina kuhudumia wateja wakorofi na wasumbufu katika maeneo yao ya kazi.
.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.