Na Elinipa Lupembe
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuŕu kitaifa ndugu Abdallah Shaib Kaim ameagiza kukamilisha madi wa maji safi na salama kukamilika kwa wakati na kufikia wananchi ili kufikia lengo la serikali la upatikanaji wa huduma za maji karibu na wananchi.
Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ameiwataka Mamlaka ya maji pindi mradi utakapokamilika, kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma hiyo ya maji kulingana na uwezo wake, kwa kuwa watu wametofautiana uwezo wa kiuchumi
"Niwatake AUWSA kuhakikisha mnaweka vituo vya kuchotea maji vya kutosha kwa wananchi wote ambao hawana uwezo wa kuingiza maji ndani ya nyumba zao, wapate huduma karibu na makazi yao" Ameagiza Kiongozi huyo
Hata hivyo wanufaika wa mradi huo, wameipongeza Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaondolea kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji safi, kero iliyodumu kwa miaka nenda rudi inayozorotesha afya na uchumi wao.
Diwani wa kata ya Oldonyosamu Mhe. Raymond Rairumbe ameishukuru serikali ya Rais Samia kwa mradi huo, mradi ambao licha kuondoa kero ya upatikanaji wa maji, amekirinkuwa maji hayo ni tiba kwao, kwa kuwa yataondoa changamoto ya matumizi ya maji yenye floraidi iliyozidi inayoathiri afya za wananchi wa maeneo hayo.
"Tunamshukuru mama Samia kwa kutukumbuka na kuletea mradi wa maji, kinamama tunateseka sana, tunatumia punda na pikipiki kuagiza maji kwa gharama kubwa, huku hakuna maji na maji yaliyopo yana madini ya floraidi ambayo inamadhara kwa afya ya binadamu na wanyama, watu wanapinda miguu, watoto wanazaliwa na vichwa vikubwa, tunashukuru sana na kumpongeza Rais wetu" Amesema
Katika mradi huo wa maji safi wa Oldonyosambu Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ameweka jiwe la Msingi kwenye Tanki la lita efu 5, mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 6.3 fedha kutoka serikali kuu, kupitia Mfuko wa maji wa Taifa na kutekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Arusha '( AUWSA)
Utekelezaji wa mradi huo umefikia 30% na unaotegemea kuondoa kero ya maji kwa wananchi 29,449 wa vijiji vya Oldonyosambu, Lemanda na Losinoni.
KAULI MBIU: " TUNZA MAZINGIRA, OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA VIUMBE HAI KWA UCHUMI WA TAIFA"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.