• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Kituo cha Afya Olkokola chapata msaada wa Kompyuta

Posted on: June 16th, 2018

Na. Elinipa Lupembe.

Shirika lisilo la kiseriksli la Ace Africa limetoa msaada wa komputa tano na lota mbili kwenye kituo cha afya cha Olkokola kata ya Lemanyata, halmashauri ya Arusha.

Vifaa hivyo ya kisasa vimetolewa,  kwa lengo la kuboresha utoaji na upatikanaji wa huduma bora za afya kupitia miundombinu wezeshi inayorahishisha uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu sahihi za wagonjwa na kituo kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Mratibu wa mradi wa shirika la Ace Africa, John Emmanuel amesema kuwa, wamekabidhi vifaa hivyo kwa ajili ya kuboresha uhifadhi na utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa kwa njia ya mtandao, kwa kutumia Komputa tano na lota mbili zenye thamani ya shilingi milioni 5.4.

Mratibu huyo, ameongeza kuwa shirika hilo linaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano, katika kuboresha miundo mbinu ya afya, na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za magonjwa ya kawaida katika maeneo yao, pindi wanapougua.

 "Komputa hizi zinatumia mtandao na server itakuwa Hospital ya Wilaya Olturumet, hivyo  itawarahisishia wauguzi kazi ya kusafiri kupeleka taarifa makao makuu kwa kutumia makaratasi, taarifa zitatumwa kupitia mfumo na ukiserve kumbukumbu yoyote, tayari mtu wa makao makuu atazioa taarifa hizo "amesisitiza John

Naye Mganga Mkuu halmashauri ya Arusha Dkt. Petro Mboya amelishukuru shirika la Ace Africa kwa kutoa vifaa hivyo muhimu, vitakavyorahisisha utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa kwa njia ya mtandao na kuwataka wahudumu wa kituo hicho kutumia komputa hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa na zaidi kuvitunza vifaa hivyo.

Mganga mkuu huyo, amewataka pia wauguzi hao kufanyakazi ya kuhudumia wagonjwa kwa weledi, kwa kuwa sasa  kazi ya kutunza na kutuma kumbukumbu imepungua, hivyo ni vema kutumia muda huo kuhudumia wagonjwa.

 "Kazi ya kusafiri kupeleka taarifa makao makuu haitakuwepo sasa, mtatuma taarifa hizo kupitia mtandao, hivyo tumieni muda huo kuhudumia wagonjwa kwa kutoa huduma iliyo bora" amesema Daktari Mboya

Olais Kiken mkazi wa Olkokola amethibitisha kuridhishwa na vifaa hivyo kwenye kituo chao cha afya na kuongeza kuwa,  anaamini sasa historia ya mgonjwa itahifadhiwa na hata akipoteza cheti hakutakuwa na kazi ya kuanza upya kujieleza.

" Huwa tunapata shida pale mgonjwa anapopoteza cheti, inamlazimu kuanza upya matibabu, lakini tumeambiwa mtandao unatunza kumbukumbu zote za mgojwa" amesema mzee Kiken

Hata hivyo wauguzi wa kituo cha Afya cha Olkokola, licha ya kulishukuru shirika la AceAfrica kwa msaada huo wameahidi kuvitunza na  kufanyia kazi vifaa hivyo ambavyo kimsingi vitawarahisishia kazi hasa katika utunzaji wa kumbukumbu muhimu za kituo na wagonjwa pia.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.