Na Elinipa Lupembe
Jamii imetakiwa kuwaandaa watoto kuwa wajasiriamali wafugaji kwa kuwaanzishia ufugaji mdogo wa sungura nyumbani ikiwa ni mkakati wa kufikia Ajenda ya10 -30 ya Kilimo Biashara.
Sungura anauwezo wa kuongeza mnyororo wa thamani, kwa mfugaji mbali na nyama na mbolea, mkojo wa sungura huuzwa kwa ajili ya dawa ya kuulia wadudu kwenye mboga mboga na matunda.
Rai hiyo imetolewa na Daktari wa Mifugo halmashauri ya Arusha Dkt. Yohana Kiwone, wakati akielezea mkakati wa kufikia Ajenda ya 10 - 30 ya Kilimo biashara, kwenye maonyesho ya kilimo Nanenane Kanda ya Kaskazini, yanayofanyika kwenye viwanja vya Themi - Njiro jijini Arusha.
Dkt. Kiwone amefafanua kuwa ili kuwa na jamii ya wafugaji wajasiriamali, wanaoendana na mabadiliko ya Sayansi na teknolojia, ni vema kuwaandaa watoto kwa kuwafundisha ufugaji wa sungura tangu wakiwa wadogo na baadaye kuendelea kuwa wafugaji wakubwa katika maisha yao ya utu uzima.
Ameongeza kuwa, tafiti zinaonyesha watoto wengi hasa wa kiume wanapenda sana sungura, wazazi na walezi tumieni fursa hiyo kuwawezesha watoto kufuga sungura nyumbani huku akisisitiza ufugaji wa sungura kuwa ni rahisi, unafanyika nyumbani kwenye eneo dogo huku sungura wakiwa na uwezo wa kuzaa watoto 8 mpaka 12 kwa uzao mmoja na wanauwezo wa kuzaa mara tano kwa mwaka.
"Watoto wanapenda sana sungura, hivyo ni rahisi kumuwezesha mtoto kufuga sungura nyumbani, ikiwa ni maandalizi ya kuwa mfugaji hapo baadaye akiwa kwenye maisha yake, sungura anabeba mimba kati ya siku 5 -35, na kuzaa watoto 8-12, ambao watauzwa na kufanyika kama chakula cha nyumbani" amesisitiza Dkt. Kiwone.
Allan Salvatory, ni mfugaji wa sungura, kitongoji cha Mbalakai ambaye amekiri kupenda sungura na wanampatia kipato ambacho hutumia kununua mahitaji yake ya shule huku wengine wakitumika kama kitoweo nyumbani.
"Mimi ninafuga sungura, niliona kwa rafikia yangu anafuga, mwisho nikamamua kununua sungura wawili na kuanza kufuga, sungura wana faida, wakikua huwa huwa nawauza, nimeambiwa mkojo wake hutumika kuulia wadudu ila bado sijaanza kuuuza huwa nawagawia watu bure". Amesema Allan
Naye Abdal Mvungi mtoto anayeishi Sekei, amekiri kuwa, ni rahisi kufuga sungura kwa kuwa mlo wao mkuu ni pumba, majani na maji na ukuaji wake huchukua muda wa miezi minane mpaka kuliwa na huuzwa kwa ahilingi elfu 10 mpaka 15 kwa sungura mmoja..
SHIRIKI SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022
JIANDAE KUHESABIWA 23.08.2022 ✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.