Na Elinipa Lupembe.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani halmashauri ya Arusha, wameiomba serikali kupitia Wizara ya Ardhi kuwaongezea eneo la ardhi hadi kufikia Ekari 3,000 kutoka Ekari 1,745 zilizokuwa zimetolewa hapo awali kwa matumizi ya wananchi wa halmashauri hiyo.
Maombi hayo yamekuja mara baada ya Afisa Mipango Miji mkoa wa Arusha, kwa niaba ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi mkoa, akijibu Azimio la Baraza hilo lililoitaka Serikali kurejesha shamba hilo kwa halmashauri ili iweze kuipangia matumizi na si Serikali Kuu.
Afisa mipango miji wa mkoa wa Arusha, Shairu Chuma ametoa majibu ya azimio hilo kwa kutoa ufafanuzi wa Serikali kupitia Wizara ya Ardhi juu ya maelekezo ya matumizi ya shamba la Tanzania Plantation, shamba ambalo Serikali ilifuta hati ya umiliki na kulirudisha serikalini.
Afisa huyo amewaelekeza Wajumbe hao kuwa, Serikali bado inaendelea kusimamia mpango wake wa matumizi ya shamba la Tanzania Plantation lenye ukubwa wa Ekari 6,176.5 mara baada ya kulitwaa na kulipa fidia ya shilingi bilioni 5.7 kwa mwekezaji na baadaye kuliweka shamba hilo chini ya Serikali Kuu.
Aidha ametoa ufafanuzi wa mpango wa matumizi ya shamba hilo kuwa ni pamoja Ekari 3,076.5 zimetengwa kwa ajili ya kilimo cha mkonge na kukabidhiwa kwa Bodi ya Mkonge, Ekari 1,355 kwa ajili ya ardhi ya Akiba hukue Ekari 1,745 zikitengwa kwa ajili ya mahitaji ya wananchi wa vijiji, vitongoji vya Bwawani pamoja na mahitaji ya Halmashauri na mkoa.
Hata hivyo Wajumbe hao wa Baraza la Madiwani walionyeshwa kutokuridhishwa na mpango huo kulazimika kuiomba serikali kubadilisha maamuza hayo na kuongezewa eneo katika shamba hilo, wakifafanua kutokana na uhitaji wa ardhi kwa wananchi wengi unatokana na uhaba wa ardhi katika maeneo ya halmashauri ya Arusha.
Akiwasilisha azimio la mkutano huo Mwenyekiti halmashauri ya Arusha, Ojung'u Salekwa, ameiomba Serikali kuiongezea halmashauri eneo la Ekari 1,225 na kufikia Ekari 3,000 kutoka Ekari 1,745 zilizokuwa zimetolewa hapo awali kwa matumizi ya wananchi.
Naye Diwani wa kata ya Mateves Freddy Lukumai amesisitiza kuiomba Serikali kuongeza eneo la shamba hilo kwa halmashauri kutoka eneo lililokiwa limetolewa kwa halmashauri hapo awali, huku akisisitiza kuomba hekima za Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kutumika katika kufanya maamuzi ya mgao huo.
Naye Diwani wa kata ya Oldonyosambu Mhe. Raymond Lairumbe, amewasilisha kilio cha wananchi wa Oldonyosambu waliotoa ardhi yao kwa ajili ya matumizi ya jeshi na serikali kuwaahidi kupewa fidia ya ardhi sehemu nyingine.
"Ninaiomba serikali kusikia kilio cha muda mrefu cha wananchi wa kata yangu ya Oldonyosambu, wananchi ambao wamekuwa wakiahidiwa mara nyingi kupewa ardhi mbadala wa ardhi waliyoito, ardhi ambayo inatumika kwa manufaa ya watanzania wote". Amesisitiza Diwani huyo Mhe. Lairumbe
Hata hivyo Afisa Mipango Miji alipokea maombi na mapendokezo yaliyotolewa na madiwani hao, na kuahidi kuyafikisha kwenye mamlaka husika za Serikali kupitia Waziri mwenye dhamana na kubainisha ukweli wa uhaba wa ardhi katika mkoa wa Arusha na kuwashauri viongozi hao kuelimisha jamii, kufanya matumizi bora ya ardhi kulingana na ufinyu wa ardhi katika maeneo yao.
ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
#KaIInaendelea✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.