Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, Bw. Seleman H. Msumi, amewahimiza wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kusoma katika Shule ya Msingi Enaboishu Academy. Amesema shule hiyo ni ya serikali na imejipambanua kwa kulea na kufundisha wanafunzi kwa kutumia mchepuo wa Kiingereza, jambo linalowaandaa watoto kuwa na uelewa mpana na ushindani katika ngazi mbalimbali za kielimu.
Aidha, Bw. Msumi amesisitiza kuwa Enaboishu Academy inatoa elimu bora yenye kuzingatia maadili, nidhamu na ubunifu, huku ufaulu wake ukiwa wa kiwango cha juu. Ameongeza kuwa uwepo wa shule hiyo ni fursa kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuhakikisha watoto wanapata malezi bora na elimu yenye ubora wa kitaifa na kimataifa.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.