Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Samia Suluhu Hassan, ameipongeza serikali ya Norway kupitia Ubalozi wa Ufalme wa nchi hiyo, nchini Tanzania, kwa kufadhili ujenzi wa miundombinu katika Chuo cha Misitu Olmotony,halmashauri ya Arusha, wilayani Arumeru.
Makamu wa Rais, ametoa pongezi hizo, mapema leo, wakati akizindua jengo la mihadhara na bweni la wanafunzi, katika Chuo cha Misitu Olmotony, na kuipongeza Serika kifalme ya Norway kwa kwa juhudi zake za kufadhili Taasisi za Elimu ya Uhifadhi wa Misitu na Mazingira.
Katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amezindua jengo la mihadhara lenye uwezo wa uwezo wa kusomesha wanafunzi takribani 240, pamoja na Bweni la wanafunzi wa kike lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 100, majengo yaliyogharimu kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 1.8, ujenzi uliofadhiliwa na Serikali ya Kifalme ya Norway kupitia Mradi wa Kujenga uwezo wa Jamii kwa njia ya mafunzo katika Usimamizi Shirikishi wa Misitu, MKUHUMI na Mabadiliko ya Tabianchi maarufu kama ECOPRC.
Makamu huyo wa Rais, amesema kuwa, majengo ni muhimu sana kwa chuo hicho, kwa kuwa yatasaidia kupunguza uhaba wa madarasa uliokuwepo, pamoja na kuimarisha ustawi wa wanafunzi wa kike licha ya waondolea adha ya kupanga nyumba za watu binafsi nje ya chuo.
Aidha Mhe, Samia ameendelea kuushukuru Ubalozi huo kwa kutoa ufadhili kwa wanafunzi 128 kimasomo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada, chuonini hapo huku wanafunzi 56 kati yao wakiwa ni wanawake.
Zaidi Mhe Samia ameushukuru mambo mengi, yaliyofanywa na Ubalozi huo ikiwa ni pamoja na kukiunganisha chuo hicho kwenye Mkongo wa Taifa, kuboresha maktaba pamoja na kukiwezesha kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya kufundishia.
Ameongeza kuwa, juhudi zote hizo zitasaidia kuimarisha mazingira ya kujifunzia, pamoja na kutoa taaluma bora, itakayowezesha kuzalisha watalaam wenye ujuzi wa kiwango cha hali ya juu.
Hata hivyo Makamu wa Rais, ameelezea changamoto ya ukataji miti hovyo na uzembe katika upandaji miti zinavyoharibu uoto wa asili na kusababisha uharibifu na mazingira ya asili, na kuzitaka taasisi husika kusimamia, kusimamia upandaji na utnzaji wa miti pamoja na kuwa na takwimu sahihi za idadi ya miti.
Awali, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga, alieleza kuwa kutokana na uhaba wa mabweni na kumbi za mihadhara, Chuo kilikuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi wachache kulingana na mahitaji, kwa kudahili wanafunzi 600 tu badala ya kudahili wanafunzi zaidi ya 1,000.
Mhe, Hasunga amesema kuwa licha ya ujenzi wa miundombinu hiyo kusaidia kuboresha utoaji wa mafunzi ya kiwango cha juu lakini pia utawezesha chuo hicho kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa.
Aidha, Naibu Waziri Hasunga, ameuomba Ufalme wa Norway kuendelea kushirikiana na Chuo hicho, ikiwemo kuendelea kuongeza mabweni ya wavulana, madarasa pamoja na kuboresha vifaa vya mafunzo ili chuo kiweze kufikia lengo lake la kuongeza udahili wa wanafunzi chuonj hapo.
Naye Balozi wa Norway nchini, Elizabeth Jacobsen amesema kuwa, lengo la nchi yake kufadhili mradi huo, ni kuimarisha ustawi wa miti na kuhakikisha, miti iliyopo haikatwi ovyo badala yake jamii ijikite zaidi katika kupanda miti, ili kuepuka majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.
Chuo cha Misitu-Olmotonyi kilianzishwa mwaka 1937, kwa madhumuni ya kufundisha elimu ya uhifadhi wa misitu kwa ngazi ya ufundi-sanifu na kimekuwa tegemeo kubwa ndani na nje ya Tanzania, hasa katika ukanda wa Kusini mwa Afrika.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.