Na Elinpa Lupembe.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, Mhe. Noah Lembris na familia yake, tayari ametimiza wajibu wake, kama Mkuu wa Kaya, kwa kuhesabiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake eneo la Ilkiushini kata ya Olturumet.
"Niwatake wananchi wote wa Arumeru Magharibi na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wamehesabiwa ili kuipa serikali nafasi ya kupanga mipango ya maendeleo kupitia Takwimu zitakazopatikana".Amesema Mbunge huyo.
Hata hivyo amewataka baadhi ya wananchi kuachana na imani potofu za kuwaficha watu wenye ulemavu, na kuhakikisha watu wote wamehesabiwa bila kujali hali walizo nazo.
Zoezi la Sensa ya watu na Makazi linaendelea katika halmashauri ya Arusha,huku kukiwa na hali ya amani na utulivu, wakazi wa halmasahuri hiyo wakiwa nyumbani kusubiri Makarani wa Sensa kufika kwenye kaya zao.
HAKIKISHA UMEHESABIWA✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.