Na. Elinipa Lupembe.
Miaka 4 ya Serikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, takribani wananchi elfu 50 wa vijiji vitano, halmashauri ya Arusha, wamefanikiwa kupata huduma za maji safi na salama, kama alivyoahidi, wakati anaingia madarakani Oktoba mwaka 2015 na kukabidhiwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Serikali kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya nchini Uingereza (DFID), wametekeleza mradi wa maji wa Vijiji Vitano, mradi utakaohudumia wananchi wa vijiji vya Olkokola, Lengijave na vitongoji vya Ngaramtoni, Seuri na Ekenywa vya Mamlaka ya Mji mdogo Ngaramtoni.
Mradi huu uliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 8.4, umesanifiwa kutumia teknolojia ya hali ya juu ya kuchuja maji, kutumia mitambo inayoondoa uchafu wote pamoja na madini hatari ya Floraidi, madini ambayo yamekuwa ni tishio kwa afya za wananchi wa maeneo hayo.
Mradi huu pia, unatumia teknolojia ya malipo ya kabla ya kabla (pre-paid), teknolojia inayotekelezwa na shirika la eWater, na kuufanya uweze kujiendesha na kudumu kwa muda wa zaidi miaka 20, mradi huu umekamilika kwa asilimia 95 na tayari baadhi ya maeneo, wananchi wameanza kupata maji kwa majaribio.
Picha ya mtambo wa kuchujia maji
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.