Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Mrisho Gambo amewakabidhi Katibu Tawala wa wilaya ya Arumeru na Mkurgenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha jumla ya mifuko 700 Saruji, mabati 200, Nondo tani 2, lita 500 za mafuta ya dizel kwa ajili ya kuendeshea mitambo pamoja na mbao ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake alizowaahidi wananchi wa Halmshauri ya Arusha wakati wa ziara yake ya siku tano ya kikazi aliyoifanya mapeam wiki iliyomaliziaka.
Mkuu wa mkoa Gambo amesema kuwa amefikia uamuzi huo wa kuchangia baada ya kuridhishwa na juhudi mbalimbali zinazofanywa na wananchi kwa kushirikiana na halmashauri katika kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya halmashauri hiyo pamoja na changamoto zilizowasilishwa na wananchi kwenye mikutano ya hadhara.
Aidha amewataka Wananchi wa halmashauri ya Arusha kujitoa katika kuchangia kujenga nchi yao kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe na kuachana na dhana ya kutegemea wageni kutoka nchi za nje.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.