Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo amewataka wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa wa Arusha kufanya maandalizi ya kutosha ya kuwapokea wanafuzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwanzoni mwa mwaka ujao 2018.
Gambo ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na benki ya NMB kanda ya Kaskazini hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Sokon II mapema wiki hii.
Awali akipokea vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 30 Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa anatambua mchango wa benki ya NMB katika maendeleo ya elimu mkoani Arusha hivyo wakurugenzi wote wanapswa kutumia misaada hiyo kwa maendeleo ya mkoa.
Amesema kuwa vifaa vilivyotolewa na benki ya NMB vitumike kufanya maandalizi ya kuwapokea wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya ujenzi Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini Salie Mlay amesema kuwa benki ya NMB ni mdau katika kuchangia huduma za jamii kwa kutumia silimia 1% ya faida inayopatikana kila mwaka.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.