Shirika la kimataifa la WaterAid Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Uingereza- DFID linategemea kuanza ujenzi mpya wa mradi wa maji katika za Oltrumet na Olkokola halmashauri ya Arusha.
Katika hatua za awali za utekelezaji wa mradi huo, Mkurugenzi wa WaterAid Tanzania Dk. Ibrahim Kabole ameongoza timu ya wataalam wa maji kutembelea eneo utakapotekelezwa mradi huo na kujionea eneo yanapopatikana maji pamoja na kuzungumza na viongozi wawakilishi wa kata hizo mbili hatimaye kukutana na kufanya mazungumzo ya mradi huo na uongozi wa halmashauri ya Arusha.
Dk. Kabole ameuelezea mradi kuwa utakuwa ni mradi tofauti na miradi mingine iliyowahi kufanyika ambao utatumia teknolojia ya kisasa ya mfumo wa kielekroniki wa kulipia Ankara za maji kabla ya kutumia yaani ‘pre paid’ pamoja na kutambua matumizi sahihi ya maji, mfumo utakaowekwa na shirika la e-waterpay.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.