Mratibu Msaidizi wa Uchaguzi Wilaya Bi Elizabeth Ngobei, amefungua kikao cha Viongozi wa Vyama vya Siasa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Arusha.
Akizungumza na Viongozi hao, pamoja na kujadili miongozo mbalimbali ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vilevile amewataka Viongozi hao wawahamasishe wananchi na wanachama wao kujitokeza kwenye zoezi la uandikishaji wa orodha ya wapiga kura inayotarajiwa kuanza Tarehe 11/10/2024 hadi tarehe 20/10/2024.
“Ndugu viongozi, tunatambua kuwa ni haki ya kila mwananchi kujiandikisha na kupata uhalali wa kuchagua viongozi wanaowataka, kama wasipojiandikisha hawatakuwa na sifa ya kupiga kura tarehe 27/11/2024”
Ikumbukwe kuwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika kila baada ya miaka mitano na kwa mwaka huu 2024 utafanyika mnamo tarehe 27 Novemba,ukitanguliwa na zoezi la kujiandikisha litakalo anza tarehe 11 Oktoba hadi 20 Oktoba 2024.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.