Mkurugenzi wa shirika la Johns Snow Ink (JSI) divisheni ya Kimataifa la nchini Marekani, Bi. Chuanpit Chuaoon, ameridhishwa na kazi zinazofanywa na timu ya watoa huduma kwenye masuala ya watoto ngazi ya jamii (Community Case Workers - CCW).
Mkurugenzi huyo, ameridhidhwa na kazi hizo, mara baada ya kukutana na timu ya CCW wanaofanya kazi ya kuhudumia watoto wenye changamoto mbalimbali za kiafya, ikiwemo wenye maambukizi ya VVU, wenye, lishe duni, wenye kufanyiwa ukatili na wale wanaoishi kwenye mzazingira hatarishi katika ngaziya jamiim ndani ya kata tano za halmashauri ya Arusha na kushuhudia matokeo ya kazi zilizofanywa na timu hizo, alipokutana nao, kwenye Ofisi ya kata ya Oloirien.
Bi. Chunpit, amesema kuwa amepata picha halisi ya huduma zinazotolewa na timu hizo za CCW, mara baada ya kupokea shuhuda za watu, walisaidiwa na timu hizo, na kufafanua kuwa, kazi zinazofanywa na timu hizo, zinasaidia kurudisha matumaini ya watu waliokuwa wamepoteza matumaini kwa kukata tamaa, pamoja na kuokoa maisha ya binadamu, yaliyokuwa kwenye hatari ya kutoweka.
"Tunahitaji maisha hata baada ya kupata changamoto, mtu anayekata tamaa anatakiwa faraja ili arudishe matumaini na kuendelea na maisha kwa kutekeleza majukumu yake ya kazi, nimefurahishwa na shuhuda za watu, waliosaidiwa kutatua changamoto zao na kurejesha matumaini huku wakiendelea kufanya majukumu yao ya kawaida" amesema Chunpit
Awali watoa huduma kwa jamii- CCW, walipata fursa ya kumuelezea mgeni huyo rasmi, kazi wanazozifanya kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kutafuta taarifa za familia zenye changamoto, kuwaorodhesha na kuanza kuwapatia huduma kwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri ya Arusha na shirika la JSI.
Catherine Tarimo, mtoa huduma kata ya Ilboru, amefafanua kuwa, wao kama timu, baada ya kujengewa uwezo na shirika la JSI, wamefanikiwa kutambua kaya zenye watoto wenye maambukizi ya VVU na kuweza kuwafuatilia na kuwasimamia, kumeza dawa za kufubaza virusi hivyo, pamoja na kuwarejesga waathirika walioacha kumeza dawa na kuwapa ushauri nasaha na kurejea kumeza.
Ameongeza kuwa, kupitia huduma hiyo wanayoitoa kwa jamii,ameweza kuzifikia kaya 15 zenye watoto 40 wenye changamoto mbalimbali, ikiwemo wenye maambukizi ya VVU, na watoto 15 kati ya hao wakihudumiwa na walezi.
Aidha ameongeza kuwa kuwa, kuna baadhi ya huduma kama za kubaini kaya na kuzisajili, ushauri na ushauri nasaha, wanazitoa wao kama timu, lakini kuna huduma za mtoto amefaniyiwa ukatili, wenye utapiamlo uliozidi na wagonjwa wapa rufaa kwenda kwenye vituo vya afaya, na waliofanyiwa ukatili hutoa taarifa kwenye ofisi za kata na Ustawu wa jamii kwa ajili ya kupata huduma za polisi na mahakama.
Naye Mkurugenzi Mtendaji, halmashauri ya Arusha, Dkt. Wilson Mahera, licha ya kushukuru na kulipongeza shirika la JSI kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano, yenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za afya na kuwafikia wananchi wote, ameahidi kujipanga kuendeleza watoa huduma hao, kwa kuendekea kuwajengea uweo ili waweze kutoa huduma hiyo muhimu kwa jamii.
Aidha, Dkt. Mahera, ameongeza kuwa, licha ya kuwa shirika hilo la JSI, linategemea kumaliza muda wake mwaka 2020, lakini bado wananchi wanauhitaji mkubwa wa huduma hizo, huku akiwataka wanufaika hao, kuto kukata tamaa na badala yake kuzingatia matumizi sahihi ya dawa na kujikita zaidi kwenye shughuli za uzakishaji mali na kusisitiza kuwa changamoto, ni sehemu ya maisha ya binadamu.
Hata hivyo Afisa Ustawi wa Jamii, halmashauri ya Arusha, Beatrice Tengi, amesema kuwa, kupitia mpango huo wa timu ya ccw, wameweza kushughulikia mashauri ya watoto walio kwenye mazingira hatarishi kwenye kaya 684, zenye jumla ya watu 2,267, kati ya hao, jumla ya watoto 1,993 walibainika kuishi katika mzangira hatarishi, na watoto 173, walibanika wana maambukizi ya VVU, wameweza kuunganishwa kwenye vituo vya Afya na kuanzishuwa dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI.
Ameongeza kuwa watoa huduma hao, walitoa rufaa 1086, na kati ya rufaa hizp, 145 ambao ninwazazi, walezi wa watoto waishio kwenye mazingira hataririshi, wameunganishwa kwenye vikundi vya uwezeshwaji kiuchumi, kwa lengo la kufanya shughuli za ujasiriamali ili kuweza kujikimu kimaisha.
Mfumo jumishi wa kushuguli mashauri ya watoto, ni mfumo wa kitaifa wenye lengo la kutoa huduma tatu, kupitia sekta ya Afya, Ustawi wa Jamii na Ulinzi kwa watoto walio katika mazingira hatarishi, walioathirika na wanaoishi na maambikizi ya Virusi vya UKIMWI, ambapo mtoa huduma amejengewa uwezo wa kuunganisha kaya zaidi ya moja kupata.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.