Na Elinipa Lupembe
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya kichama Aruemru, ndugu Simoni Ole Saning'o na familia yake, tayari ametimiza wajibu wake, kama Mkuu wa Kaya, kwa kuhesabiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake eneo la Ilkerini kata ya Kisongo.
Mwenyekiti Saning'o amekiri kufurahishwa na zoezi hilo kwa kuwa maswali ndani ya dodoso, ni maswali yanayoeleweka na kujibika kwa urahisi na kuwataka wananchi hususani jamii ya wafugaji kutoa ushirikiano kwa Makarani hao wa Sensa ya watu na Makazi kwa kutoa taarifa sahihi zinazohitajika na serikali.
"Zoezi la Sensa ni zoezi muhimu sana kwa watanzania na Taifa kwa ujumla, uwepo wa takwimu sahihi za watu na makazi zitaiwezesha serikali kupanga mipango sahihi kulingana na idadi ya watu" Amesisitiza Saning'o
Zoezi la Sensa ya watu na Makazi linaendelea katika halmashauri ya Arusha,huku kukiwa na hali ya amani na utulivu, wakazi wa halmasahuri hiyo wakiwa nyumbani kusubiri Makarani wa Sensa kufika kwenye kaya zao.
HAKIKISHA UMEHESABIWA✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.