Mwenyekiti wa Baraza la Mamlaka ya Mji Mdogo Ngaramtoni mheshimiwa Elias Munis ameonesha matumaini makubwa juu ya upatikanaji wa huduma ya Maji kwa wananchi na wakazi wa Mamlaka hiyo na vitongoji vyake ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2018.
Mwenyekiti huyo amesema hayo alipozungumza na mwandishi wetu mara baada ya kufunga Mkutano wa Baraza la Mamlaka hiyo la kujadili taarifa za utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2017/18 .
Mwenyekiti Munisi amesema kuwa Mamlaka inamatumaini makubwa kuwa miradi ya maji inayotekelezwa katika mamlaka hiyo pindi itakapokamilika itapunguza adha ya maji inayowakabili wananchi wa Mamlaka hiyo kwa muda mrefu sasa.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.