Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Arusha, Mwl. Hossein Mghewa, anawakumbusha wananchi wote kujiandikisha kwenye Orodha ya Wapiga Kura, Zoezi linaendelea mpaka tarehe 14/10/2019.
Tumia vizuri muda uliopangwa, hakikisha umejiandikisha ili upate Sifa ya kupiga Kura kuchagua Mwenyekiti wa Kitongoji, Mwenyekiti wa Kijiji na Wajumbe wa Serikali ya Kijiji.
SIFA ZA MPIGA KURA
1. Awe Raia wa Tanzania.
2. Awe na umri wa miaka 18
3. Awe mkazi wa eneo husika
4. Awe na akili timamu
Nenda ukajiandikishe kwenye Kituo kilivyoainishwa kwenye Kitongoji chako.
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.