Na Elinipa Lupembe
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa amewataka Makarani wa Sensa kuacha tabia ya kupiga picha na kurekodi video wakati wanapofanya mahojiano na watu wakati wa Sensa ya watu na makazi kwa kuwa ni kosa kisheria.
Dkt. Albina amesema hayo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya zoezi la sensa ya watu na makazi mkoani Iringa, amefafanua kuwa adhabu anayostahili Karani aliyetendakosa hilo ni faini ya shilingi milioni 2, kifungo cha miezi sita au vyote kwa pamoja.
"NI kinyume cha sheria kwa Karani yeyote kufanya hivyo kwa kuwa taarifa hizo ni siri, makarani watakaofanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria" Amefafanua Mtakwimu Mkuu wa Serikali
Aidha amebainisha kuwa tayari wameanza kuwachukulia hatua baadhi ya makrani waliofanya makosa hayo kulingana na sheria na kuwataka Makarani hao kutokufanya kosa hilo kwa kuwa ninkinyume cha sheria na taratibu za zoezi la Sensa.
Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi lilianza rasmi usiku wa kuamkia tarehe 23.08.2022 na linategemea kukamilika siku saba baadaye, kwa wale ambao bado hawajahesabiwa wahakikishe wanahesabiwa na wanaotoka nyumbani, wanashauriwa kuacha tarifa zao nyumbani hivyo kila mtua natakiwa kutoa ushirikiano kwa karani wa Sensa kwa kutoa taarifa zote zonazohitajika kwa kuwa taarifa hizo ni siri
SOURCE: Mwananchi Instragram
ZIMEBAKI SIKU MBILI
HAKIKISHA UMEHESABIWA ✍✍
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.