• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Arusha District Council
Arusha District Council

Serikali ya jamuhuri ya Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Makuu
    • Mikkati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara na Vitengo
      • Utawala na Utumishi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Fadha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliji
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Works
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo na Umwagiliaji na Ushirika
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Internal Audit
      • Nyuki
      • Uchaguzi
      • UKIMWI/ AIDS
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Livestock
    • Wadau wa Maendeleo
  • Huduma Zetu
    • Health
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Utawala Fedha na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili ya Madiwani
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Vikao vya Timu ya Uendeshji ya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mktaba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa UMMA
    • Video za Shoghuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Pentekoste Ngulelo, watoa zabihu ya chakula kwa wanafunzi kidato cha nne Arusha DC

Posted on: October 30th, 2019

Na. Elinipa Lupembe.

Kufuatia mkakati wa kuendelea kupandisha kiwango cha taaluma na kuongeza ufaulu wa mitihani ya Taifa ya kidato cha nne, halmashauri ya Arusha imefanikiwa kupata  chakula kwaajili ya wanafunzi wa kidato  cha nne, katika kipindi chote cha mitihani ya Taifa inayotarajiwa kuanza mapema mwanzoni mwa wiki ijayo.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo wa chakula, kutoka Kanisa la Pentekoste- Ngulelo, Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Alvera Ndabagoye, licha ya kushukuru waumini wa kanisa hilo, amesema kuwa, uhakika wa uwepo wa chakula kwa wanafunzi, kipindi chote cha mtihani, utawawezesha wanafunzi, kutulia kisaikolojia na kufanya vizuri katika matokeo yao ya mitihani hiyo.

Ameongeza kuwa, halmashauri inatambua na kuthamini mchango wa wadau wote, kutokana na uhalisia kuwa, Serikali peke yake haiwezi kutatua matatizo yote yanayoikabili sekta ya elimu, hivyo amewataka wadau kuendelea kujitoa kwa hali na mali kuunga mkono juhudi za aserikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Rais John Pombe Makufuli kwa kutoa elimu bila malipo.

Awali, Kiongozi wa Huduma ya Mwalimu aonesmo ya Kanisa la Pentekoste Ngulelo, mwalimu Onesmo Anael, amesema kuwa, waumini wa kanisa lake, wameamua kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano,  kupitia Sera ya Elimu bila malipo na kuwa jukumu la chakula ni la wazazi, na kuamua kuwasaidia wazazi wasio na uwezo, kuwapa watoto hao chakula, kipindi chote cha kufanya mitihani ya Taifa mwaka 2019.

Amefafanua kuwa, wapo watoto yatima, wanaoshindwa kumudu kuchangia chakula shuleni, lakini pia wapo watoto ambao, wazazi wao hushindwa kuwachangia chakula cha mchana wawapo shuleni, kutokana na kipato chao kidogo, na kusababisha watoto wao kushinda bila kula wawapo shuleni.


"Kama kanisa, tumeguswa na hilo, tukaamua kuelekeza sadaka zetu, kwa wanafunzi wote wanaotegemea kuanza mitihani yao ya kidato cha nne wiki ijayo, kwa shule za ndani ya hamashauri yetu ya Arusha"amesema Mwalimu na mtumishi Onesmo.


Mtumishi Onesmo, ameweka wazi kuwa, waumini wa kanisa lake, wamekusanya sadaka zao na kutoa jumla ya magunia 40 ya mahindi yenye kilo 100 na mifuko 20 ya maharage, kwa pamoja vikawasidie wanafunzi wetu wa kidato cha nne.


Naye Afisa Elimu Sekondari, Medard Lupenza, amethibitisha kuwa, kiasi hicho cha mahindi na maharagwe, kimegawanywa kwenye shule 26 za serikali zenye wanafunzi wa kidato cha nne, kwa uwiano kulingana na  idadi ya wanafunzi.


Hata hivyo, wakuu wa shule zote 26, wamewashukuru uongozi wa kanisa la Pentekoste Ngulelo, pamoja na waumini wote, kwa kutambua na kuguswa na changamoto ya chakula, inayowakabili wanafunzi wasio na uwezo,  na  kuamua kujitoa kuchangia chakula ili kuwapa nafasi walimu na wanafunzi kufikiria mirihani tu.


Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa shule hao, Mwenyekiti wa Wakuu wa shule, Mwalimu Mwamvita Kilonzo, amesema kuwa walimu,  hupata wakati mgumu sana pale ambapo, wazazi hushindwa kiwalipia watoto wao chakula, jambo ambalo husababisha unyonge kwa watoto wasiokula shuleni na kuwafanya hata walimu kujisikia vibaya.

Hata hivyo, mwalimu Kilonzo, amesema kuwa, uhakika wa  uwepo wa chakula, utasababisha utulivu kwa walimu na wanafunzi, na kutegemea ufaulu kuongeza kwa wanafunzi hao, wa kidato cha nne mwaka huu wa 2019.



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA ENABOISHU FM - ARUSHA DC May 26, 2025
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2023 ARUSHA DC June 11, 2023
  • ZIARA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS TAMISEMI, MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA 17 SEPTEMBA 2024 September 13, 2024
  • MTIHANI WA DARASA LA SABA 11-12/09/2024 September 09, 2024
  • Tazama zote

Habari mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA CHAKULA BORA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAPEWA ELIMU YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    May 27, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA

    May 26, 2025
  • RC MAKONDA ATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA ARUSHA

    May 25, 2025
  • Tazama zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vinavyoingiliana

  • Leseni ya vileo
  • Fomu ya ukaguzi

Viunganishi vinavyohusiana

  • Tovuti kuu ya serikali
  • Tamisemi
  • Utumishi portal
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Mkoa wa arusha
  • ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Sekei Road

    Anuani ya posta: 2330 Arusha

    Simu : +255 027 2502737

    Simu: 073 65000476

    Barua pepe: ded@arushadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.