Na Elinipa Lupembe
Serikali ya awamu ya sita kupitia Mfuko wa Maendleeo ya Jamii (TASAF) imefanikisha ujenzi wa Zahanati mpya Kijiji cha Engutukoit Kata ya Oldonyowas Halmashauri ya Arusha kwa gharama ya shilingi milioni 102.
Ujenzi wa zahanati hiyo, umefanyika kufuatia mkakati wa Serikali ya kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ili kukabiliana na vifo vya wanawake na watoto.
Ujenzi wa zahanati hiyo, utasaidia kuokoa maisha ya wakazi wa kijiji hicho hususani kina mama wajawazito na watoto ambao hapo awali walitembea umbali mrefu kutafuta huduma za Afya huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa kukosa huduma za haraka.
Wakizungumzia kwa hisia baadhi ya wakazi wa Engutukoit wakati ujenzi wa zahanati ukiendelea,
wamesema kuwa, zahanati hiyo itakuwa ni mkombozi wa akina mama wajawazito kujifungulia sehemu salama badala ya kujifungulia nyumbani kama ilivyokuwa hapo awali.
Wamesema kuwa, wajawazito walilazimika kujifungulia nyumbani jambo ambalo lilihatarisha maisha yao na watoto, huku watoto wa chini ya miaka 5 wakishindwa kuhudhuria kliniki kwa usahihi kutokana na kushindwa kumudu gharama za usafiri kwa kila mwezi.
“Tulikuwa tunapata shida sana endapo ikitokea dharura ya mgonjwa nyakati za usiku, ilitulazimu kukodi pikipiki kwa shilingi elfu 30 kumpeleka mgojwa kupata matibabu kwenye kata jirani ya Oldonyosambu, lakini sasa tunafurahi kwa kuwa tutapata huduma za afya hapa karibu na nyumbani.” Ameweka wazi Jackline Saruni.
Hata hivyo wananchi hao wameishukuru sana Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia TASAF kwa kuwakumbuka na kuwajengea zahanati hiyo kwani walikaa miaka mingi bila kupata huduma hiyo muhimu katika kijiji chao.
"ARUSHA DC ni Yetu, Tushirikiane Kuijenga"
Sekei Road
Anuani ya posta: 2330 Arusha
Simu : +255 027 2502737
Simu: 073 65000476
Barua pepe: ded@arushadc.go.tz
Copyright ©2018 Arushadc . All rights reserved.